Fullshangwe Blog, Bungeni Dodoma

Mbunge wa Hanang, Asia Halamga ameipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa hatua na mikakati inayoendelea kuchochea maendeleo ya sekta ya utalii nchini, akisema kuwa mafanikio yaliyopatikana yamechangia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi wa taifa.

Akizungumza bungeni jijini Dodoma leo Mei 18, 2026 wakati wa mjadala wa bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027, Halamga amesema Serikali imefanya kazi kubwa katika kuhakikisha sekta ya utalii inakua kwa kasi kupitia kuimarisha vivutio vya asili na kuongeza ufanisi wa utangazaji wa Tanzania kimataifa.

Ameongeza kuwa mafanikio hayo yamechangia kuongeza ajira kwa wananchi, kuongeza mapato ya taifa na kuinua hadhi ya Tanzania katika ramani ya utalii duniani, hatua inayopaswa kupongezwa na kuendelezwa zaidi kwa mikakati madhubuti.

Katika mchango wake, mbunge huyo amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuwekeza katika hifadhi za taifa na vivutio vya asili ili kuhakikisha Tanzania inaendelea kuvutia wageni wengi zaidi kutoka ndani na nje ya nchi.

Aidha, Halamga ameahidi kuendelea kuiunga mkono Serikali katika juhudi za kukuza sekta ya utalii kwa maslahi mapana ya taifa.