Na Happy Lazaro, Arusha
Tanzania imejipanga kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji ili kuvutia wawekezaji zaidi kutoka Urusi na mataifa mengine duniani kwa lengo la kukuza uchumi wa viwanda na maendeleo endelevu.
Hayo yamesemwa leo jijini Arusha na NAIBU Waziri wa Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Dkt. Pius Chaya, akifungua Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Urusi lililowakutanisha zaidi ya kampuni 120 kutoka Urusi pamoja na wadau wa sekta binafsi na serikali kutoka Tanzania.
Katika hotuba yake leo mei 15,2026, amewashukuru Wizara ya Maendeleo ya Uchumi ya Urusi, Ubalozi wa Urusi nchini Tanzania, Russia Congress Foundation, Russian Export Center, Mamlaka ya Uwekezaji na Kanda Maalum za Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Zanzibar Investment Promotion Agency (ZIPA), Tanzania Private.
Amesema kongamano hilo limekuja wakati muafaka ambapo Tanzania inaendelea kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inayolenga kuifanya nchi kuwa uchumi wa kisasa unaotegemea viwanda, teknolojia, ubunifu na unaoongozwa na sekta binafsi.
“Tanzania ipo katika kipindi muhimu cha mageuzi makubwa ya uchumi chini ya uongozi wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ambapo serikali imeendelea kufanya maboresho makubwa ya mazingira ya biashara, kuimarisha miundombinu na kuvutia uwekezaji wa ndani na nje,” amesema .
Dkt. Chaya amesema kuwa serikali ina matumaini makubwa kuwa kongamano hilo litafungua njia mpya za biashara, uwekezaji, mwa utalii,ΔΊ uhamishaji wa teknolojia na maendeleo ya pamoja kati ya Tanzania.