‎Na Meleka Kulwa-Fullshangwe Blog, Bungeni Dodoma

Serikali imeendelea kuboresha huduma za matibabu ya ubingwa na ubingwa bobezi katika hospitali za rufaa nchini ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma hizo ndani ya nchi.

Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa , amesema kuwa katika kipindi cha mwaka 2021/2022 hadi Machi 2026 wagonjwa 170 walifanyiwa upandikizaji wa figo huku wagonjwa 57 wakifanyiwa upandikizaji wa uloto.

‎Akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo , Mei 11, 2026,  bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amebainisha kuwa wagonjwa 1,791 walifanyiwa upandikizaji wa nyonga na magoti huku wagonjwa 1,688 wakifanyiwa upasuaji wa mgongo.

Pia ameongeza kuwa wagonjwa 2,074 walifanyiwa kuzibua mishipa ya moyo huku wagonjwa wengine wakipata huduma mbalimbali za ubingwa bobezi nchini.

Amesema kuwa wagonjwa 731 wa saratani walifanyiwa uchunguzi kwa kutumia PET-CT Scan huku maelfu wengine wakipata tiba ya mionzi na immunotherapy. 

Aidha amesema kuwa uwekezaji huo umewezesha wananchi kupata huduma ndani ya nchi na kuvutia wagonjwa kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika.