Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) (kushoto), akisalimiana na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Denis Londo (Mb), mara baada ya kufika katika mpaka wa Tanzania na Zambia kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Tano wa Kamati ya Pamoja ya Biashara (5th Joint Trade Committee – JTC) kati ya Tanzania na Zambia, uliofanyika katika Mkoa wa Songwe-Tunduma, mpakani mwa Tanzania na Zambia.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), akiteta jambo na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uchambuzi wa Sera, Wizara ya Fedha, Bw. William Mhoja, wakati wakijiandaa kuingia na kushiriki, Mkutano wa Tano wa Kamati ya Pamoja ya Biashara (5th Joint Trade Committee – JTC) kati ya Tanzania na Zambia, uliofanyika katika Mkoa wa Songwe eneo la Tunduma, mpakani mwa Tanzania na Zambia.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), akifuatilia Mkutano wa Tano wa Kamati ya Pamoja ya Biashara (5th Joint Trade Committee – JTC) kati ya Tanzania na Zambia, uliyofanyika katika Mkoa wa Songwe, eneo la Tunduma, mpakani mwa Tanzania na Zambia.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Denis Londo (Mb), akizungumza wakati wa kufunga Mkutano wa Tano wa Kamati ya Pamoja ya Biashara (5th Joint Trade Committee – JTC) kati ya Tanzania na Zambia, uliyofanyika katika Mkoa wa Songwe-Tunduma, mpakani mwa Tanzania na Zambia.
Viongozi mbalimbali wakiwemo Naibu Mawaziri, kutoka wizara mbalimbali za Serikali ya Jamhuri ya Muungani wa Tanzania na Serikali ya Zambia wakimsikiliza Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Denis Londo (Mb) (hayupo pichani), akizungumza wakati wa kufunga Mkutano wa Tano wa Kamati ya Pamoja ya Biashara (5th Joint Trade Committee – JTC) kati ya Tanzania na Zambia, uliofanyika katika Mkoa wa Songwe eneo la Tunduma, mpakani mwa Tanzania na Zambia.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), (wapili kulia), Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Denis Londo (Mb) (katikati), wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine kutoka Serikali ya Tanzania na Zambia, baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Tano wa Kamati ya Pamoja ya Biashara (5th Joint Trade Committee – JTC) kati ya Tanzania na Zambia, uliofanyika Mjini Tunduma, mpakani mwa Tanzania na Zambia, Mkoa wa Songwe.

Picha za matukio mbalimbali ya Mkutano wa Tano wa Kamati ya Pamoja ya Biashara (5th Joint Trade Committee – JTC) kati ya Tanzania na Zambia, uliyofanyika katika Mjini Tunduma, mpakani mwa Tanzania na Zambia, Mkoa wa Songwe. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF – Tunduma)
………
Na Asia Singano, WF – Tunduma
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), ameshiriki Mkutano wa Tano wa Kamati ya Pamoja ya Biashara (5th Joint Trade Committee – JTC) kati ya Tanzania na Zambia, uliofanyika Mjini Tunduma, Mpakani mwa Tanzania na Zambia, katika Mkoa wa Songwe, ambapo wamejadili kwa kina namna ya kukuza biashara kwa faida ya nchi hizo mbili.
Katika mkutano huo pande zote mbili zilijadili kuhusu namna ya kuboresha mazingira ya biashara na miundombinu yake ikiwemo sekta ya usafirishaji itakayochochea ufanyaji biashara na kutoa fursa zaidi kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa nchi zote mbili.
Mkutano huo ulitanguliwa na kikao cha ngazi ya Wataalamu, na kufuatiwa na kikao cha ngazi ya Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali ikiwemo Wizara ya Fedha, Wizara ya Uchukuzi, Wizara ya Viwanda na Biashara Pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Zambia.
Viongozi wengine wa Serikali ya Tanzania walioshiriki Mkutano huo ni Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile (Mb), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. James Millya (Mb), Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Denis Londo (Mb), pamoja na viongozi wengine waandamizi kutoka Serikali ya Zambia.
