Na. Meleka Kulwa- Fullshangwe Blog, Bungeni Dodoma 

 Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeiomba Serikali kuidhinisha jumla ya takribani Sh trilioni 2.3 kwa ajili ya kuimarisha sekta ya elimu nchini, ikilenga kuboresha miundombinu, kuongeza ubora wa ufundishaji na kuendeleza matumizi ya teknolojia katika elimu.

Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo Mei 7,2026 bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema fedha hizo zitaelekezwa katika miradi ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa madarasa, mabweni, maabara, vyuo vya ufundi pamoja na ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia.

Amesema kuwa Serikali inaendelea kuipa kipaumbele sekta ya elimu kutokana na mchango wake mkubwa katika kujenga rasilimali watu wenye ujuzi na uwezo wa kuchangia katika uchumi wa taifa.

Aidha, amebainisha kuwa sehemu kubwa ya fedha hizo itaelekezwa kwenye miradi ya maendeleo ili kuhakikisha wanafunzi wote nchini wanapata mazingira bora ya kujifunzia bila changamoto za msingi.