Na. Meleka Kulwa-Fullshangwe Blog, Bungeni Dodoma
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa Serikali imeendelea kuwekeza katika maendeleo ya vijana kupitia mpango wa Samia Scholarship Extended DS/AI+ unaolenga kuwajengea uwezo katika masuala ya akili unde na sayansi data.
Amesema kuwa wanafunzi 50 wenye ufaulu wa juu katika masomo ya sayansi walichaguliwa kupata ufadhili wa masomo nje ya nchi katika vyuo vikuu vya kimataifa vinavyobobea katika teknolojia za kisasa.
Akiwasilisha Bajeti ya Wizara ya Elimu kwa Mwaka 2026/2027 Mei 7,2026, Waziri Wa Elimu, Prof. Adolf Mkenda, amebainisha kuwa baadhi ya wanafunzi hao tayari wameanza masomo nchini Afrika Kusini huku wengine wakitarajiwa kwenda nchini Ireland kuendelea na masomo yao katika fani za akili unde, sayansi data na teknolojia shirikishi.
Pia ameongeza kuwa mpango huo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuandaa wataalamu wa Kitanzania watakaoweza kushindana katika soko la ajira la kimataifa na kusaidia maendeleo ya teknolojia nchini.
