6 May 2026, 12:26 pm

Afisa wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji akionyesha namna ambavyo jeshi hilo hufanya kazi ya uokoaji. Picha na Kale Chongela

Jumla ya matukio 82 yameripotiwa katika kipindi cha miezi mitano ndani ya mkoa wa Geita ambapo kati ya matukio hayo, 32 ni ya moto huku operesheni 50 zikiwa za uokoaji

Na: Kale Chongela

Watu 32 wamefariki dunia kwa kipindi cha miezi mitano ya mwaka 2026 mkoani Geita, kufuatia kuongezeka kwa matukio ya moto na uokoaji yaliyoacha athari kubwa kwa jamii.

Takwimu hizo zimetolewa Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Geita, Keneth Mwakasitu katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wazima Moto Duniani ambapo jumla ya matukio 82 yameripotiwa katika kipindi hicho ambapo amesema kati ya matukio hayo, 32 ni ya moto huku operesheni 50 zikiwa za uokoaji huku majeruhi wakiwa 69.

Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakionesha kwa vitendo namna gani wanavyofanya kazi ya kuzima moto kwa kutumia vifaa vyao. 

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela akiwa katika maadhimisho hayo katika viwanja vya shule ya msingi Ludete mamlaka ya mji mdogo wa Katoro wilayani Geita amesema licha ya changamoto hizo uwepo wa vifaa vya kisasa umeongeza ufanisi wa uokoaji na kusaidia kupunguza madhara yanayotokana na majanga.

Hata hivyo baadhi ya wanaanchi walioshiriki maadhimisho hayo wamepongeza Jeshi hilo kwa kuridhia maadhimisho hayo kufanyika katika kata ya Lutede yaliyoaambatana na Utoaji wa Elimu ya namna ya kukabilian na majanga ikiwemo moto na ajali.