Meneja Biashara wa Samsung Electronics Tanzania, Bw. Daesong Ra (kushoto) akizindua rasmi duka jipya la kampuni hiyo Jijini Dodoma. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Mauzo wa bidhaa za mkononi wa Samsung Electronics East Africa (Tanzania) Bw. Mgope Kiwanga na katikati ni wamiliki wa duka hilo.

……….

Samsung Electronics East Africa imeendelea kutanua wigo wake nchini kwa kuzindua rasmi duka jipya Jijini Dodoma kwa ushirikiano na mbia wake wa rejareja, F & S

Duka hili jipya ni sehemu ya juhudi zinazoendelea za Samsung za kusogeza bidhaa na huduma zake karibu na wateja kote nchini Tanzania.

Duka la Dodoma limeanzishwa ili kuwapa wateja uzoefu kamili wa Samsung mahali pamoja. Linajumuisha vifaa vya mkononi na vifaa vya kielektroniki vya nyumbani katika eneo moja, likiwawezesha Watanzania kuona jinsi bidhaa za Samsung Electronics zinavyofanya kazi kwa pamoja ili kuleta mfumo wa kisasa wa kidijitali uliounganishwa.

Uzinduzi huo rasmi ulihudhuriwa na Meneja Biashara wa Samsung Electronics Tanzania, Bw. Daesong Ra na wabia wengine muhimu jambo linalosisitiza umuhimu wa uwekezaji huu katika ukuaji wa teknolojia nchini Tanzania.

Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo ya Vifaa vya Mkononi wa Samsung Electronics East Africa (Tanzania), Mgope Kiwanga, alisema: “Uzinduzi wa duka hili jipya unaonyesha dhamira ya muda mrefu ya Samsung ya kuleta na kupanua uvumbuzi kwa walaji katika soko la Tanzania. Hii ni hatua muhimu kwetu, kwani tunataka wateja wengi zaidi wapate bidhaa zetu kwa urahisi na wajionee jinsi zinavyofanya kazi kwa pamoja ili kurahisisha maisha ya kila siku na kuwa yenye muunganiko zaidi.”

Duka la Chapa ya Samsung limeanzishwa ili kuwapa wateja uzoefu wa vitendo na wa mwingiliano zaidi. Wageni wanaweza kuchunguza simu za kisasa za Samsung Galaxy, vishikwambi (tablets), vifaa vya kuvaa mwilini, TV, vifaa vya nyumbani, na vifuasi (accessories), huku wakijionea jinsi vifaa mbalimbali vinavyounganishwa na kufanya kazi kwa pamoja.

Wateja wanaweza pia kujaribu bidhaa ndani ya duka, kupata msaada kutoka kwa wafanyakazi wa Samsung, na kupata huduma za baada ya mauzo. Lengo ni kuhakikisha kwamba wateja hawanunui tu bidhaa, bali pia wanaelewa jinsi ya kuzitumia kikamilifu.

Mgope aliongeza: “Kuzinduliwa kwa duka hili Dodoma kunaonyesha imani yetu katika soko la Tanzania. Uwekezaji kama huu unasaidia kuboresha upatikanaji wa teknolojia, kutengeneza ajira, na kusaidia ukuzaji wa ujuzi. Pamoja na kuboresha upatikanaji wa huduma kwa wateja, duka hili pia linatengeneza fursa za ajira na kusaidia kujenga ujuzi wa ndani. Samsung imetoa mafunzo kwa wafanyakazi wa hapa nchini ili kuhakikisha wateja wanapata msaada na huduma sahihi.”

Uzinduzi wa duka la Chapa ya Samsung Dodoma unasisitiza dhamira ya Samsung Electronics East Africa kwa Tanzania na maono yake ya kuwezesha maisha ya kisasa yenye muunganiko wa kidijitali, kwa kuweka uvumbuzi na uzoefu wa mteja kuwa kipaumbele katika utendaji wake.