Na Happy Lazaro ,Arusha.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla amewasili Mkoani Arusha leo kupitia uwanja wa ndege wa Arusha kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Joseph Mkude kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla.
Mhe. Abdulla anatarajiwa kufungua Kongamano la Idhaa za Kiswahili duniani, Kongamano litakalozinduliwa kesho kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC Jijini Arusha.
Katika mapokezi hayo Mhe. Abdullah amepokelewa pia na Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Mhe. Paul Makonda.

