Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Anna Athanas Paul akisisitiza jambo wakati akijibu maswali ya Waandishi wa Habari alipozungumzia Mafanikio na Maendeleo ya Wizara kutimia Siku Mia Moja za Uongozi wa Awamu ya Nane ya Rais Dk Hussein Ali Mwinyi hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Habari Maelezo Rahaleo Zanzibar

Mkurugenzi wa Habari Maelezo Salum Ramadhan Abdalla akitoa hotuba ya makaribisho katika Mkutano wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Waandishi wa Habari kuzungumzia Mafanikio na Maendeleo ya Wizara kutimia Siku Mia Moja za Uongozi wa Awamu ya Nane ya Rais Dk Hussein Ali Mwinyi hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Habari Maelezo Rahaleo Zanzibar.

Mwandishi wa Habari wa ZC TV Abbas Al-sabri akiuliza Maswali katika Mkutano wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto alipozungumzia Mafanikio na Maendeleo ya Wizara kutimia Siku Mia Moja za Uongozi wa Awamu ya Nane ya Rais Dk Hussein Ali Mwinyi hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Habari Maelezo Rahaleo Zanzibar.
…………
Na Maelezo Zanzibar 03.03.2026.
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinasia, Wazee na Watoto imeanzisha mradi wa Dkt. Mwinyi Busting Fund kwa ajili ya kuwafikia na kuwainua wanawake na wajasiri amali wadodo ili kujiinua kichumi.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Rahaleo Zanzibar kuhusu Siku 100 za Mafanikio ya Uongozi wa Dkt. Mwinyi Waziri wa Wizara hiyo Anna Athanas Paul, amesema Program hiyo inalengo la kuwawezesha wanawake na kuinua mitaji yao ya kujiendeleza kwa kipata mikopo isiyo na riba.
Amesema mradi huo umewanufaisha zaidi ya wajasiriamali 69 na ambao wamejiunga katika vikundi vyao ambapo zaidi ya vikundi 6000 Unguja na Pemba ambapo wamepewa mkopo wa sh. Laki tano kila mwanachama ili kujiimarisha katika biashara zao.’
“Hapa tuliwalenga wajasiriamali wadogo wadogo kama vili wauza mikate wauza chapati ili wao ndio wanufaike na mkopo huo ambao hauna riba na tuliweka zisizo na masharti magumu ili wapate kunufaika na mkopo huo na usio na riba” alieleza.
Aidha Waziri Anna amesema kuwa Wizara pia umeweza kuimarisha mifumo ya unyanyasaji wa kinjisia ikiwemo kuimarisha madawati ya jinsia katika kila Wilaya ili kuhakikisha kuwa vitendo vya udhalilishaji viapunua nchini.
“Tumeunda madawati ya kijinsia katika vikosi vya SMZ ikiwemo kikosi cha JKU na KMKM ili kuwajua Watoto wanafika katika maeneo hayo wanapopata matatizo kujua kesi zao zinapelekwa maeneo hayo kutokana na sehemu Watoto wengi hutumia na tunahakikisha kila kikosi kina madawati yetu ili wananchi waweze kuyatumia madawati yetu”, amefahamisha.
Aidha amefahamisha kuwa wameweza kutoa uelewa kuhusiana vitendo vya udhalilishaji wa wanawake na Watoto pamoja na kutoa kwa wanaume juu ya kuwashirikisha katika kukuza usawa wa kijinsia na kuwa na mabadiko.
Akizungumzia kuhusiana na uimarisha wa haki za Watoto Waziri Anna amefahamisha kuwa katika kuadhimisha siku 16 za mtoto jumla ya kesi 50 za watoto ikiwemo makosa ya 43 jinai na 7 madai zimeripotiwa katika mahkama za Wilaya Unguja na Pemba kati ya hizo kesi 9 zimetolewa hukumu ambapo kesi 8 za jinai na moja ya madai.
Aidha amesema jumla ya kesi 212 za utelekezaji zimeripotiwa katika vituo mbalimbali katika za Unguja na Pemba ambazo zinatokana na Watoto wanakosa huduma na kupata haki zao za msingi ambazo zimekuwa nyingi katika jamii.
Aidha amesema wizara inaendelea kuwahamasisha wazazi kuwalea Watoto katika mazingira mazuri ili waweze kupata haki zao za msingi ili kuwaweka katika hali ya amani na maisha salama.
“Tatizo la utelekezaji wa Watoto linasababshwa na wazazi kuachana na kupelekea Watoto kuachwa kwa mzazi mmoja ambapo mama huachiwa Watoto pekee bila ya kupatiwa huduma hivyo Wizara inawahasisha wazazi kuwalea Watoto katika mazingira bora na salama”, ameeleza Waziri Anna.
Kwa upande wa Pensheni Jamii Waziri huyo ameeleza Wizara inaendelea kuhakiki wazee ili kuhakikisha wanapata stahiki zao kila kwa kila aliyefikia pamoja na kutoa vitambulisho kwa ajili ya kupata huduma za kijamii kwa urahisi.
Hata hivyo amesema Idara ya Maendeleo ya Jamii imeandaa sera yake ambayo itakuwa ni sera ya awali na itakuwa na maendeleo mazuri katika jamii kwa kuhusisha wanajamii wote.



