Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na Viongozi na Wananchi mbali mbali waliohudhuria katika Iftari aliyowaandalia iliyofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.

…………………………

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla amewataka wananchi wa Zanzibar kuendelea kudumisha Amani na Utulivu uliopo chini ili kuiwezesha serikali kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Ameyasema hayo mara baada ya Iftari aliyowaandalia viongozi na wananchi mbali mbali wa Zanzibar iliyofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idris Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.

Amesema Amani na mshikamano ndio chemchem ya maendeleo katika Taifa lolote lile duniani hivyo kila mtu kwa nafasi yake analazimika kuhubiri na kuilinda Amani iliyopo nchini kwa nyakati zote kwa maslahi mapana ya vizazi vilivyopo na vianavyokuja.

Aidha, Mhe. Hemed amewashukuru wanachi kwa heshima kubwa waliyompatia ya kuitikia mwaliko wake na kuungana nae katika Iftari hio jambo ambalo linadhihirisha uwepo wa umoja na mshikamano kwa Wazanzibari.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Mohamed Ali Abdalla amemshukuru Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa kuendeleza utamaduni wake wa kuwakutanisha pamoja viongozi na wananchi mbali mbali katika Iftari jambo linalozidisha mapenzi baina yao.

Mhe. Mohammed amewapongeza viongozi wakuu wa Kitaifa kwa kuendelea kuliongoza Taifa kwa Mafanikio makubwa kutokana na maono yao mapana na busara wanazozitumia katika kuwaletea maendeleo Watanzania.