………
NA DENIS MLOWE, IRINGA
MBUNGE wa jimbo la Kilolo, Dkt. Ritta Enespher Kabati ameomba shule shikizi ya Madizini kufunguliwa mapema ili kusaidia watoto kusoma karibu.
Kabati ameomba hayo wakati wa ziara yake ya kushiriki ujenzi wa choo cha walimu katika shule hiyo iliyopo kata ya Ilula tarehe 24 Februari 2026.
Kabati ametaka kikwazo cha kukosekana choo cha walimu kiondolewe ili shule hiyo iweze kuanza mapema huku utaratibu wa ujenzi wa choo cha walimu ukiendelea.
Amesema shule hiyo inaweza inatakiwa kuzinduliwa kabla ya tarehe 7 Machi 2026 ili kuondoa adha wanayopata watoto wa darasa la kwanza na la pili wanaosoma mbali katika shule ya Msingi Isoriwaya.