Mkurugenzi wa Kampuni ya Wailes Frank Ndunguru,akizungumza na wanafunzi na walimu wa Shule ya Sekondari Mbinga Day,kabla ya kuanza kwa zoezi la upandaji miti ya kivuli na matunda shuleni hapo,katikati Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Ramia Mganga(Picha na Muhidin Amri).

Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mbinga Day Halmashauri ya Mji Mbinga Mkoani Ruvuma,wakiwa wameshika miti ya matunda  iliyotolewa na Kampuni ya Wailes  yenye makao makuu yake Mkoani Ruvuma akwa ajili ya kupandwa shueni hapo(Picha na Muhidin Amri).

Mkurugenzi wa Kampuni ya Wailes Frank Ndunguru kulia,akizungumza na wanafunzi,walimu na baadhi ya wakazi wa Mji wa Mbinga wakati wa zoezi la upandamiti miti katika shule ya Sekondari Mbinga Day Wilayani Mbinga, ikiwa ni jitihada za Kampuni hiyo katika kuhifadhi mazingira,kulia kwake Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Ramia Mganga(Picha na Muhidin Amri)

Mkurugenzi wa Kampuni ya Wailes Frank Ndunguru,akipanda miti  wa matunda kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Mbinga Day Wilayani Mbinga,ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan za kuhifadhi mazingira hapa Nchini(Picha na Muhidin Amri.

Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Kamishina Msaidizi  Ramia Mganga,akipanda mti wa matunda kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Mbinga Day Wilayani Mbinga iliyotolewa na Kampuni ya Wailes  kama kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za uhifadhi wa mazingira hapa Nchini(Picha na Muhidin Amri)

……………..

Na Mwandishi Wetu,Mbinga

WATANZANI wametakiwa kuendelea kuunga mkono jitihada za Rais Samia Samia Suluhu Hassan,  katika uhifadhi wa mazingira kwa kupanda miti kwa wingi  kwenye maeneo yaliyoharibiwa na shughuli za kibinadamu ili kusaidia kurudisha uoto wa asili na kutunza vyanzo vya maji vyenye faida kubwa kwa maisha yao.

Wito huo umetolewa jana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Wailes yenye makao makuu Wilaya ya Mbinga Mkaoni Ruvuma Frank Ndunguru, wakati wa uzinduzi wa zoezi la upandaji miti kwa shule za Sekondari na maeneo ya wazi katika Halmashauri ya Mji Mbinga uliofanyika katika Shule ya Seondari Mbinga Day.

Ndunguru alisema,suala la kuhifadhi mazingira sio la Serikali pekee bali wadau wote wanatakiwa kuungana pamoja ili kurudisha uoto wa asili ambao kwa kiasi kikubwa umechangiwa na shughuli mbalimbali za kibinadamu ikiwemo kilimo.

Alisema,wakati haraka za kibinadamu za kujitafutia ridhiki zikiendelea kufanyika zimekuwa chanzo kikubwa cha uchafuzi wa mazingira na kusababisha nchi kupata hasara kubwa ya kutumia fedha nyingi ili kuyarejesha maeneo hayo katika hali ya kawaida.

Amewataka wanafunzi na walimu wa shule hiyo,kuendelea kuelimisha jamii na wananchi wafahamu umuhimu wa kupanda miti na kuepuka kukata miti ovyo bali kupanda na kuitunza ili ikue hatua itakayosaidia kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Alieleza umuhimu wa kupanda kama njia mojawapo ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na miti ina mchango mkubwa katika kuhifadhi ikolojia na kuboresha maisha ya binadamu.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Kamishina msaidizi wa Polisi Ramia Mganga,ameipongeza Kampuni ya Wailes kwa maono yake na kutambua umuhimu wa upandaji miti kwenye shule  na maeneo ya wazi kwani litasaidia sana wanafunzi na jamii yetu kuwa na mazingira mazuri ya kujifunzia.

Mganga,ameshauri kampuni hiyo kugawa na  kupanda zaidi miti ya matunda ili wanafunzi na jamii ya wana Mbinga waweze kula matunda kwa wingi ambayo ni muhimu kwa afya za binadamu.

Amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika kusimamia na kuhifadhi mazingira nchini kwa vitendo na kusisitiza kuwa jukumu la kuhifadhi mazingira ni la kila mmoja.

Mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Mbinga Ikupa Erasto alisema,zoezi la upandaji miti  wamelipokea kwa furaja kubwa kwa sababu miti hiyo itawasaidia kuongeza na kupata hewa safi pamoja na kuwa na mazingira safi na salama.

Ikupa,alisema kuwa yeye na wanafunzi wenzake watahakikisha wanatunza miti hiyo ili iweze kukua vizuri na kustawi kwa faida ya yao na wanafunzi wengine watakaokuja kusoma katika shule hiyo.

Mwanafunzi mwingine Magreth Komba alisema,zoezi la upandaji miti katika shule hiyo ni zuri kwani litasaidia kupata hewa safi na kupata matunda ambayo yatawezesha kuboresha afya zao.

Kwa mwaka 2026 Kampuni ya Wailes imeweka lengo la upanda miti zaidi ya 10,000 ya matunda,kivuli na mbao kwenye shule mbalimbali za Sekondari Wilayani Mbinga ikiwa ni mkakati wake wa kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhifadhi mazingira.