Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla akiwasalimia Waumini wa Dini ya kiislam katika Masjid AFRAA BINT ISSA (MASJID SHURBA) uliopo Kidongo Chekundu Wilaya ya Mjini Unguja mara baada ya Swala ya Ijumaa.
……….,…
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla amewataka Waumini wa dini ya kiislamu kuendelea kuwasaidia watu wenye mahiaji maalumu hasa katika kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa ramadhani ili kuweza kupata radhi za allah ( S.W) pamoja na kufikia lengo ramadhani.
Ameyasema hayo wakati akiwasalimia waumini wa Masjid AFRAA BINT ISSA ( MASJID SHURBA) uliopo KIDONGO CHEKUNDU Wilaya ya Mjini Unguja mara baada ya kumaliza Ibada ya swala ya Ijumaaa.
Amesema suala la kusaidiana na kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu wakiwemo wajanae, mayatima, watu wenye ulemavu na wasiojiweza hujenga umoja, upendo na mshikamano na kuweka usawa miongoni mwao.
Alhajj Hemed amefahamisha kuwa mwezi wa ramadhani ni mwezi wa kuchuma thawabu kupitia njia mbali mbali ikiwemo kukithirisha kufanya ibada, kuwafikia wenye uhitaji kwa kutoa zaka na sadaka.
Amewataka waumini wa dini ya kiislamu kuzilinfa funga zao kwa kuepuka mattendo yote yanayotengua funga sambamba na kuwasisitiza kuzidisha kufanya ibada hasa wakati wa usiku ili kuweza kujikurubisha kwa M.Mumgu na kupata fadhila za mwezi huu mtukufu wa ramadhan.
Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewasisitiza waumini wa dini ya kiislam na wazanzibar kwa ujumla kuendelea kuitunza amani na utulivu uliopo nchini ili kuisaiidia serikali kufanya yale yote iliyoyakusudia kwa wananchi wake.
Amesema kuwepo kwa maendeleo nchini kunabitaji uwepo wa amani na utulivu hivyo ni wajibu wa kila mmoja wetu kwa nafasi yake kuitunza na kuinadi amani kwa wakati wote.
Akitoa khutuba ya swala ya Ijumaa Ustadh MOHAMMED SOUD amewataka waislamu kudhidhibiti nafsi zao kutokana na matamanio jna kujiepusha na vishawishi mbali mbali vitakavyopelekea kutengua guzo za funga na kutofikia lengo la funga kwao.
Ustadhi MOHAMMED amewasisistiza waumini wa dini ya kiislam kujikurubisha kwa Allah ( S.W ) kwa kusoma sana Qur-an, kusimama itikafu pamoja na kuwasaidia watu wasio na uwezo wakiwemo mayatima na wajane.

