Mkurugenzi wa Tiba Hospitali ya Qualitas Kigamboni Dkt. Jane Manyahi akionesha tuzo ya tuzo ya Cheti cha ubora kilichotolewa na Jukwaa la afya Tanzania (Tanzania Healthy Summit ) THS , kupitia Programu ya Safe Care.
‎

Rais wa Jukwaa la afya Tanzania (Tanzania Healthy Summit ) THS Dkt Omary Chillo akihutubia wakati wa hafla fupi ya kukabidhi tuzo ya cheti cha utoaji huduma Bora.


‎Baadhi ya wafanyakazi wa Hospital ya Qualitas wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi katika hafla ya utoaji tuzo ya cheti cha Ubora.
‎
‎……….

Jukwaa la Afya Tanzania (Tanzania Healthy Summit – THS) limesema kuwa ili kupata matokeo chanya katika utoaji wa huduma bora za afya, kuna haja kwa mamlaka za Serikali na sekta binafsi kuendelea kuunganisha nguvu kwa pamoja katika kuimarisha miundombinu ya utoaji wa huduma za afya kwa wananchi.

‎Hayo yamebainishwa na Rais wa Jukwaa hilo, Dkt. Omary Chillo wakati wa hafla fupi ya kukabidhi tuzo ya cheti cha utoaji huduma Bora iliyofikia hadhi ya nyota nne katika Hospitali ya Qualitas iliyopo Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.

‎Aidha Dakta Chilo ametumia jukwaa hilo kueleza umuhimu wa kuongeza ubora katika vituo vya afya nchini, huku aliongeza kuwa ubora wa utoaji wa huduma za afya unaoanzia hadhi ya nyota moja hadi tano ni sehemu ya utekelezaji wa ajenda ya jukwaa la afya Tanzania THS, kupitia Programu ya Safe Care inayo hamasisha watoa huduma za afya wa Sekta na binafsi na za umma kujikita kutoa huduma zinazo kidhi viwango vya kitaifa na kimataifa.

‎Amesema Taasisi hiyo moja ya malengo yake makubwa ni kuimarisha huduma za Afya hapa nchini katika kusimamia majukumu yake wamegundua changamoto mbalimbali ikiwemo Utawala, miundombinu ya majengo, wafanyakazi na katika hayo wameendelea kutoa ushauri ilikuboresha hali hiyo.

‎Pamoja nahayo ametoa wito kwa hospitali na vituo vya afya Umma na binafsi kote nchini kufanya tathimini ya ubora wa huduma wanazotoa ili kufanya kuboresha

‎Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tiba Hospitali ya Qualitas Kigamboni Dkt. Jane Manyahi, ameshauri hospitali na vituo vya afya kujiunga katika taasisi hiyo ambayo inatoa tathimini za huduma za afya ili kujenga imani kwa watu.

‎‘’Ninayofuraha kubwa sana siku ya leo kwa kupokea tuzo au cheti hiki cha ubora ngazi nne yaani Nyota nne na sisi kwetu hii ni kitu kikubwa kwa sababu tunaposema ubora katika utoaji huduma ni muhimu sana kwa maana huduma hizi zinakuwa salama kwa pande zote mbili kwa mgonjwa na mtoa huduma na tuanshukuru sana Mungu kwa kufika hatua hii”Alisema

‎‘’Wateja wetu pia wanapoonakuwa Hospitali yetu imefanyiwa tathimini na kupata cheti wanaongeza imani yao kwetu kwa kuwa tunatoa huduma bora na za kuaminika”Alisema

‎Nao baadhi ya wagonjwa waliofika kupata huduma ya matibabu katika Hospitali hiyo wakiongozwa na Esther Mickison, wameshukuru uongozi wa Qualitas kwa kusimamia huduma bora kwa wakazi wa Kigamboni na Dar es salaam kwa ujumla , huku wakisisitiza watumishi kuendelea kufanya kazi kwa weledi ili kulinda Afya za wagonjwa