Mkurugenzi kuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Seif Abdalla Juma akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali kuhusiana na  Taarifa isio sahihi iliotoka katika Mitandao ya kuharibiwa pamoja na  kuibiwa Baadhi ya Mizigo ya Abiria wanaoshuka Katika Uwanja Huo jambo ambalo sio la kweli na halina Ushahidi,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Taminal 3 Uwanja wa Ndege zanzibar.

Baadhi ya Vyombo vya Habari Vilivyohudhuria katika Mkutano wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Seif Abdalla Juma na  kuzungumzia Taarifa isio sahihi iliotoka katika Mitandao kuhusiana na kuharibiwa pamoja na  kuibiwa Baadhi ya Mizigo ya Abiria wanaoshuka Katika Uwanja Huo jambo ambalo sio la kweli na halina Ushahidi,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Taminal 3 Uwanja wa Ndege zanzibar.

Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Mkutano wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Seif Abdalla Juma  kuzungumzia Taarifa isio sahihi iliotoka katika Mitandao kuhusiana na kuharibiwa pamoja na  kuibiwa Baadhi ya Mizigo ya Abiria wanaoshuka Katika Uwanja Huo jambo ambalo sio la kweli na halina Ushahidi,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Taminal 3 Uwanja wa Ndege zanzibar.
……………..

Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar imesema kuwa hakuna ushahidi uliyopatikana unaonesha uwepo wa wizi kwa baadhi ya mizogo katika viwanja hivyo

Akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake Uwanja wa Ndege wa Amani Abeid Karume Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo
 Seif Abdallah Juma amesema kuwa suala hilo halijabainika kutokana na Uchunguzi uliyofanywa
Aidha amesema kuwa kufuatia kadhia hiyo Mamlaka imechukua hatua za kuunda Kamati ya kufanya uchunguzi pamoja na kuwataka wachukuzi wa mizogo hiyo kuvaa kamera ili kubaini vitendo vyovyote vya wizi
Amesema kuwa Mamlaka imepokea malalamiko Desemba 29 mwezi uliyopita kwa baadhi ya wafanya biashara kuhusiana na kufunguliwa kwa baadhi ya mizigo yao jambo ambalo limetia wasi wasi na kupelekea kundwa kwa Kamati hiyo
Aidha amefahamisha kuwa katika kufanya uchunguzi huo Kamati imebaini uwepo wa zaidi ya  mizogo 100 imekuja tayari imefunguliwa ambapo baadhi ya mizigo hiyo imeharibika
Akizungumzia kuhusu kamera za kuchunguzia ameeleza kuwa katika Ndege eneo linalowekwa mizogo hakuna kamera hivyo ni vigumu kuona knachofanyika huko
Ameongeza kuwa katika kuhakikisha usalama wa mizigo  Mkurugenzi Mkuu amesema kuwa watu wa usalama wana haki ya kufungua mzigo na kuangalia kwa lengo la kuimarisha usalama wa abiria na mizigo
Kikao hicho kimefanyika kufuatia tuhuma za wizi zilizotolewa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari zilizokuja hivi karibuni.