Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kuimarisha ulinzi na usalama kuelekea mkesha wa mwaka mpya na sherehe za mwaka mpya kwa kufanya doria na misako katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya.
Akizungumza Disemba 31, 2025 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya SACP Benjamin Kuzaga wakati akiwa katika operesheni maalum ya kuzuia na kudhibiti makosa ya usalama barabarani katika barabara kuu ya Mbeya – Kyela amesema kuwa, Jeshi hilo lipo imara kuhakikisha linazuia na kudhibiti makosa yote ya uhalifu.
Aidha, Kamanda Kuzaga amesema kuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuchoma moto matairi barabarani wala kupiga/kulipua baruti au fataki bila kibali, watakaofanya hivyo ni wale tu walioomba kibali na kuruhusiwa chini ya uangalizi wa Jeshi la Polisi.
