…….

Na Rahma Khamis,  Maelezo Zanzibar

Wananchi wametakiwa kufuata taratibu, kanuni na Sheria za ujenzi Ili kuipunguzia gharama Serikali wakati inapotaka kufanya miradi ya Maendeleo.
MWENYEKITI WA Bodi ya Wakurugenzi WAKALA WA Majengo Zanzibar Mhandisi Mohammed Aboud Mohammed meyasema  hayo wakati akizungumza na waandishi  wa habari kando ya kikao cha Bodi hiyo kilichofanyika Ofisi za ZBA Amani viwanda vidogovidogo.
Amesema kuwa uzoefu unaonesha kuwa watu hujenga bila idhini wala vibali Rasmi  vya  Serikali Jambo ambalo linaleta athari mbeleni sio Tu kuharibu ardhi lakini pia inaigharimu Serikali na  kutumia fedha nyingi kulipa fidia Kwa wananchi waliojenga kwenye maeneo yaliopangwa Kwa ajili ya mieadi ya maendeleo.
Aidha amempongeza Dk Mwinyi Kwa Kazi anayoifanya Katika kuleta Maendeleo ya Nchi na  Kuleta maisha Bora  wazanzibar na watanzania Kwa ujumla.
Ameeleza kuwa Bodi hiyo itaendelea kutoa ushauri kwa Serikali na kusimamia  katika kuhakikisha miradi hiyo inafanikishwa Kwa Kiwango chenye ubora katika masuala mbali mbali ya Ujenzi  wa miradi ya kimkakati inayoleta mabadiliko ya Kimaendeleo Nchini.
Ameongeza kuwa miradi inayotekelezwa inatoa nafasi kubwa ya ajira na  shughuli mbalimbali za maendeleo kutokea  na kuwezesha shughuli za uchumi na Kukuza kipato cha mtu kutokana na harakati mbalimbali.
Mwenyekiti huyo amebainisha kuwa wataendelea kusimamia maeneo yote ya majenzi ya Miradi mbalimbali kuhakikisha
ujenzi unafanyika Kwa utaratibu mzuri na kukuidhi viwango vunavyotakiwa kimataifa na ubora WA Hali ya juuu
Mkurungezi Mtendaji WAKALA WA majengo Zanzibar Mhandisi Kassim Ali Omar aliishauri Serikali kuwafanyia upembuzi yakinifu baadhi ya wakandarasi na washauri elekezi wanaoshindwa kwenda sambamba na Serikali na kupelekea kutofikia malengo yiyokusudiwa  kwa wakati sahihil.
“Serikali kuwaangalia vyema wakandarasi na washauri elekezi wenye Tabia za  kuharibu  miradi ya Serikali  kwa Kuchelewesha kukamilisha miradi na kufanya miradi isiyo na viwango.”alisema
Aidha alieleza kuwa Katika miradi wanayoisimamia watahakikisha majengo yote yanakuwa na mazingira rafiki kukuidhi mahitaji ya watu wenye mahitaji maalum
 Bodi ya Wakurugenzi WAKALA WA Majengo Zanzibar imeanzishwa 2017 kwa lengo la kusimamia na kushauri Serikali katika majenzi.