Naibu waziri wa fedha Mhandisi Mshamu Ally Munde akifungua kongamano hilo jijini Arusha leo 

Happy Lazaro,ARUSHA .

Arusha .Naibu waziri wa fedha Mhandisi Mshamu Ally Munde amesema kuwa, sekta ya manunuzi nchini ni muhimu kutiliwa mkazo kwa kuwa takribani asilimia 70 ya bajeti ya serikali,inatumika kwenye maswala ya manunuzi na ugavi.

Ameyasema hayo leo jijini Arusha wakati akifungua kongamano la 16 la.mwaka la watalamu wa ununuzi na ugavi linalofanyika jijini Arusha .

Amesema kuwa, sekta hiyo ni uti wa mgongo wa nchi hivyo ni muhimu ikaboreshwa ili kupunguza hasara zinazopatikana pindi manunuzi yanapofanyika kinyume na Sheria na taratibu za manunuzi nchini.

 “Ndugu zangu wataalamu niwasihi sana muongeze umakini zingatieni sheria za manunuzi kwa kuwa mnafahamu miradi yote ya serikali hufanyika kwa kuzingatia sheria za manunuzi sasa tunapofanya kinyume na sheria hizi au taratibu mnakwamisha miradi hiyo pamoja na kusababisha hasara kwa nchi .”amesema .

Aidha amewaahidi watalaamu hao wa sekta ya manunuzi na ugavi kuwa serikali itashughulikia changamoto kubwa ya maslahi yao kwa kufikisha kwa waziri wa fedha ili waweze kufanya kazi katika mazingira rafiki na kuletea nchi maendeleo.

Aidha amewataka wataalamu wa ununuzi na ugavi nchini kutoka sekta binafsi na umma kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa kuzingatia matakwa ya sheria yaliyopo ili manunuzi yaweze kufanyika kwa weledi .

Hata hivyo amewataka waajiri kutumia wataalamu hao katika shughuli zao na wahakikishe wamesajiliwa na bodi hiyo kwani itasaidia kuleta weledi na utendaji kazi hapa nchini.

“Naziagiza taasisi zote na sekta binafsi kuzungatia matakwa ya sheria kuhusu ununuzi na ugavi hapa nchini na naiagiza bodi iendelee kufanya ukaguzi binafsi ili kuweza kudhibiti wale wanaofanya kazi kinyume cha sheria. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya (psptb) Jacob Kibona amesema kuwa,bodi hiyo ina majukumu mbalimbali.ikiwemo ya kudhibiti ubora wa taaluma hiyo ,kuendeleza mafunzo pamoja na semina katika sehemu zao za kazi.

Amesema kuwa wamekuwa wakitoa mafunzo hayo kwa kuzingatia maadili ya kitaaluma ambapo wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa fedha pamoja na kuwepo kwa maslahi madogo kwa watalaamu ikilinganisha na taaluma zingine ambapo kimekuwa ni kilio cha muda mrefu kwa wataalamu hao .