Na Hellen Mtereko,

Mwanza

Katibu wa Itikadi,Uenezi na Mafunzo Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenani Labani Kihongosi amekutana na makundi mbalimbali Jijini Mwanza kwaajili ya kutoa mrejesho wa maendeleo ya kampeni za mgombea Urais wa chama hicho.

Kihongosi amekutana na makundi hayo Leo Jumatatu Oktoba 27, 2025 katika ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu Jijini Mwanza.

Amesema kampeni hizo zilianza Agosti 28, 2025 katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe Jijini Dar es salaam ambapo kesho inatimia miezi miwili tangu safari ya kuizunguka nchi nzima.

“Sisi Chama Cha Mapinduzi katika mikutano ya kampeni za Uchaguzi Mkuu 2025, tumeweka rekodi kubwa ya mahudhurio kuwahi kutokea Takriban watu 25.3 milioni, wamehudhuria mikutano yetu ya hadhara, wakati watu 57.1 milioni, wamefuatilia kampeni zetu kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, ndani na nje ya nchi. Namba za kimtandao zinaonesha kuwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kipindi cha kampeni, amefuatiliwa mara 164.9 milioni kupitia majukwaa mbalimbali”, amesema Kihongosi

Aidha, ametoa shukurani kwa mamilioni ya Watanzania walioacha shughuli zao na kujumuika nao kwenye mikutano ya kampeni, pia tunajivunia teknolojia ya mawasiliano maana imekuwa rahisi kuwafikia watu wengi waliotufuatilia kupitia redio, televisheni, magazeti, mitandao kwa simu, kompyuta na vifaa vyote vya kidigitali, ndani ya vyombo vya usafiri, vibanda umiza, nyumbani sebuleni, baa na mabango barabarani. tumewafikia Watanzania wengi haijawahi kutokea.

Amesema mgombea Urais ameshafanya mikutano 112 ya kampeni yote imekuwa na mafanikio makubwa mikutano mikubwa viwanjani, msafara wa mgombea wetu, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kusimamishwa njiani na wananchi, hivyo kulazimika kuhutubia akiwa kwenye gari.

Wingi wa watu kujitokeza kutaka kumsikiliza mgombea wetu ni tafsiri ya imani kubwa ya watu kwa CCM na upendo mkubwa kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kutokana na uongozi wake unaojali utu na matokeo aliyoyaonesha.

Ameeleza kuwa katika mikutano yote siyo tu Dkt. Samia Suluhu Hassan, alinadi Ilani ya CCM na kutoa ahadi zake, aliwasikiliza pia wananchi usikivu huo uliwezesha kuhuisha ahadi zake kwa muhula ujao.

“Mgombea wetu wa Urais amefanya kazi kubwa ya kuinadi Ilani ya CCM ambapo hadi kufikia sasa tunauhakika watanzania wameielewa na wengi wao wapo tayari kukichagua Chama cha Mapinduzi kwa sababu Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu tumekuwa na Ilani bora kabisa ya uchaguzi,zaidi chama chetu ndiyo kimebeba matumaini ya kweli ya Watanzania”, amesema Kihongosi

Amesema Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2025 ni ya kipekee na inamanufaa makubwa kwa watanzania kwani ni Ilani inayowagusa watanzania Kila eneo kuanzia vijana ambao ndiyo moyo wa nchi,wanawake walezi wa taifa,makundi maalum,watoto,wazee na watu wenye ulemavu pia inaingia mpaka kwenye familia palipo na kitovu Cha uhenzi wa maadili ya Taifa.

Aidha, ameeleza kuwa Ilani ya CCM inatoa mwanga wa ajira na ustawi wa jamii pia inaketa suluhisho kubwa sekta ya afya.

“Ilani ya CCM ni Mwanzo wa mwisho wa kero ya maji na tunakwenda kuwa na Gridi ya maji ya Taifa,pia tunakwenda kuzalisha umeme megawati 8,000 mara mbili zaidi ya umeme tulionao Sasa”,