Wanakagera wamejitokeza kwa wingi wakiwa na shangwe , nderemo na vifijo kumlaki Dkt. Samia Suluhu Hassan, mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiongozi shupavu na Injinia wa maendeleo alie waletea maendeleo lukuki ndani ya muda mfupi wa Uongozi wake mkoani Kagera 

Wanasema hawajawahi kuona kasi ya maendeleo kama hii ya miradi ya miundombinu, huduma za jamii, uwezeshaji wa vijana na wanawake, yote yakiwa ni alama ya uongozi wenye matendo, si maneno.