SHAMRASHAMRA: Wananchi wa Uvinza wakiwa katika shamrashamra kabla ya kuanza kwa mkutano wa kampeni wa CCM katika mji wa Kazuramimba wilayani Uvinza mkoani Kigoma ambapo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan atawahutubia wananchi hao na kuwaomba kura za ndiyo katika uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025 nchini kote.