WAAPA KUMPOKEA KWA HESHIMA, KIBABE NA KISHINDO KIKUBWA

NI KWA NEEMA 10 ADHIMU ALIZOZITEKELEZA KATIKA MKOA HUO

Uchambuzi wa neema hizo.

Anaandika Mshititi Dkt. Ahmad Sovu

Mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa nafasi ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye anaendelea na kampeni za kusaka kura, anatarajiwa kuwasili mkoa wa Kigoma kuanzia tarehe 13 ya mwezi huu wa Septemba 2025.

Udadisi wa Mshtiti katika mitaa na viunga vya mji anuwai wa Kigoma umeonesha namna wananchi walivyo na ari, shauku, hamu na ghamu ya kumpokea mgombea huyo shupavu na imara katika siasa za Tanzania. ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

NEEMA ZAKE KUU 10 KWA WANA KIGOMA

Wananchi hao wameeleza kinagaubaga kuwa, kura ambazo watazirundika (kupiga kwa wingi) ni za Rais Dkt. Samia.

Wamesema Mama Samia tangu amekuwa Rais amewafanyia mambo makubwa mengi na bado wana matarajio makubwa kwake katika kuyakamilisha.

โ€œKwa mapenzi na mahaba makubwa kwa Rais Samia yanayotokana na jitihada zake kubwa za kuuletea maendeleo mkoa wa Kigoma, tutamlipa kwa mapokezi ya heshima, kibabe na kishindo,โ€ alisema mmoja wa wakazi wa mkoa huo.

Neema ya 1: Kuufanya mkoa wa Kigoma kuwa kitovu cha biashara katika ukanda huu wa Magharibi na maziwa makuu

Tangu aingie madarakani, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha wazi dhamira ya kuufanya mkoa wa Kigoma sio tu kuwa kituo cha biashara, bali kitovu cha biashara kwa ukanda wa Magharibi kutokana na jiografia yake. Serikali tayari imeunganisha mkoa wa Kigoma kwenye gridi ya Taifa, imejenga meli mpya, barabara na kuboresha kiwanja cha ndege cha Kigoma. ๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

Neema ya 2: Ujenzi wa vyuo vikuu

Rais Samia amemwaga fedha katika ujenzi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Tiba Muhimbili (MUHAS), Chuo cha Uhasibu (TIA) na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT). Vyuo hivi vitaleta chachu ya elimu, kuchagiza mzunguko wa uchumi na kuongeza ajira.

Neema ya 3: Maboresho ya Hospitali ya Rufaa Maweni na ujenzi wa Hospitali ya Kanda

Rais Samia ameongeza bajeti ya maboresho ya Maweni na anatarajiwa kujenga hospitali ya rufaa ya kanda ili kuimarisha huduma za afya.

Neema ya 4: Ujenzi wa Shule ya Kisasa ya Wasichana Kigoma Girls

Ili kuhakikisha elimu bora kwa vijana, Rais Samia amejenga shule ya kisasa wilayani Uvinza yenye hadhi ya kitaifa. ๐Ÿ‘๐Ÿ‘

Neema ya 5: Ujenzi wa barabara na soko la kisasa la Mwanga

Rais Samia amewezesha ujenzi wa barabara za njia nne, bandari ya Kibirizi na Ujiji pamoja na soko la kisasa Mwanga.

Neema ya 6: Ujenzi wa kituo cha pamoja Mnanira Kigoma

Rais Samia aliahidi kujenga one stop center Mnanira ili kurahisisha huduma kati ya Tanzania na nchi jirani. Tayari mkandarasi yupo eneo la mradi na kazi inaendelea. ๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘

Neema ya 7: Mradi wa Bonde la Luiche

Ili kukuza kilimo cha umwagiliaji, serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni 60 kufanikisha mradi huo.

Neema ya 8: Kuunganisha Kigoma na gridi ya Taifa

Katika kufanikisha azma ya Kigoma kuwa kitovu cha uchumi, mkoa wote tayari umeunganishwa na gridi ya Taifa.

Neema ya 9: Vitambulisho vya Taifa (NIDA)

Rais Samia ametimiza ahadi ya utoaji wa vitambulisho vya Taifa ambapo wananchi wengi tayari wamepata.

Neema ya 10: Ukarabati wa uwanja wa ndege wa Kigoma na ujenzi wa soko la Katonga kupitia mradi wa TACTIC

Kupitia diplomasia ya kiuchumi, Kigoma imenufaika na mradi wa TACTIC ambapo:

1. Shilingi bilioni 9.2 zitajenga na kukarabati soko la Mwanga na Katonga.

2. Shilingi bilioni 3.2 zinaendelea kugharamia upanuzi wa barabara ya Wafipa Kagera na ujenzi wa daraja la Mto Luiche.

3. Shilingi bilioni 8.6 zinaendelea kujenga barabara ya Bangweโ€“Ujiji (km 7.5).

4. Shilingi bilioni 7.5 zinatumika kujenga barabara ya Old Kasulu (km 6.5 kwa kiwango cha lami)

5. Shilingi bilioni 5.6 zinajenga mifereji ya kupitisha maji katika mitaa ya Bangwe, Burega, Rutale, Mlole, Bushabani, Mjimwema pamoja na Katonyanga.

Hizi ndizo baadhi ya neema 10 za Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkoa wa Kigoma.

Kwa neema hizi, wana Kigoma wamesema watampokea kibabe na kwa heshima Dkt. Samia. Ifikapo Oktoba 29 โœ…โœ…โœ… kura zao zote zitakuwa kwake na kwa wagombea wa CCM.

Wananchi wana matarajio zaidi ya:

Ukamilishaji wa ukarabati wa meli ya Mv. Liemba, mwongozo na ujenzi wa cherezo.

Ujenzi wa barabara ya Mpandaโ€“Kigoma.

Uhakika wa utulivu katika shughuli za uvuvi Ziwa Tanganyika.

Kuchapuka kwa biashara na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na nchi jirani.

TURASHASHE, KARIBU KWAKO KIGOMA. NJOO KIFUA MBELE MAMA, WAHA NA WAMANYEMA WENZIO WAPO READY KU โœ…

Karibu tena Kigoma, Pwani ya Bara. ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

โœ๏ธ [email protected] | 0713400079

KAZI IENDELEEE.