Na Neema Mtuka Sumbawanga
Rukwa :Mgombea mwenza wa kiti cha urais kupitia chama cha mapinduzi CCM amesema chama kimejikita katika kugusa sekta ambazo zinakwenda kuukuza uchumi wa wananchi hasa vijana.
Nchimbi amesema katika miaka mitano iliyopita serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania imejiwekeza katika nyanja mbalimbali kama sekta ya afya ,elimu , miundombinu ya barabara za lami mjini na Vijijini kutoka q1kilomita 39.4 hadi 46.5 pamoja na sekta ya uvuvi.
Akizungumza leo Septemba 9 ,2025 Nchimbi amesema malengo ya chama cha mapinduzi ni kuboresha maisha ya watanzania na kuwa na taifa lenye kujitegemea.
Pia Nchimbi amezungumzia maendeleo yaliyofanywa na rais Dkt Samia Suluhu Hassan ikiwemo uboreshaji wa bandari ya kasanga ,uwanja wa ndege ,sanjari na kutoa mikopo kwa makundi maalumu.
Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi amesema chama kimejipanga kusimamia na kuimarisha huduma za afya kwa akina mama wajawazito na watoto ili kudhibiti na kumaliza vifo vya akina mama wakati wa uzazi kutoka asilimia 9 hadi 4.
Amesema watapunguza udumavu kwa watoto wa chini ya miaka mitanona kuongeza huduma za lishe kwa makundi yanayoathirika zaidi ikiwa ni pamoja na watoto, wajawazito na vijana balehe.
“Licha ya mkoa wa Rukwa kulima mazao ya chakula na biashara lakini changamoto ya udumavu ni kwa asilimia 49.8 ambapo tutahakikisha tunapunguza tatizo.”amesema Nchimbi
Kwa upande wake Mwenyekiti mstaafu wa chama cha mapinduzi mkoa wa Ruvuma ambaye ameambatana na mgombea mwenza wa urais Hamis Ally amesema chama cha mapinduzi kina mikakati ya kudhibiti ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto,wasichana, wanawake,wazee na watu wenye ulemavu.
Akimkaribisha mgombea mwenza wa urais Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Rukwa Siraf Maufi amesema wataimarisha huduma za ustawi kwa wazee ikiwamo huduma za afya matunzo na ushirikishwaji katika maamuzi na shughuli mbalimbali za maendeleo.
Nao baadhi ya wananchi na wanachama waliojitokeza kusikiliza sera za chama cha mapinduzi ( CCM) akiwemo Agnes lyoba amesema anawaomba wagombea kutimiza yale ambayo wanaahidi ili waendelee kuaminika.
“Niombe tu wagombea kutimiza ahadi zao sio kuongea tu ili wapate kura bali tunatamani kuona utekelezaji wake.

