Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi alipowasili kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma kumwakilisha  Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kilele cha Wiki ya Utumishi wa Umma, Juni 23, 2025.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mwandishi wa Taarifa Rasmi za Bunge, Patson Sobha alipotembelea banda la maonesho la Bunge  alipomwakilisha  Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Kilele cha Wiki ya Utumishi wa Umma  kwenye Viwanja vya Chanangali jijini Dodoma, Juni 23, 2025.  Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachaweni. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurungenzi Mtendaji wa Watumishi Housing, Stephanie Solomon (wa tatu kushoto) alipotembelea banda la maonesho la Watumishi Housing wakati alipomwakilisha  Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Kilele cha Wiki ya Utumishi wa Umma  kwenye Viwanja vya Chanangali jijini Dodoma, Juni 23, 2025.  Wa pili kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza, Afisa Tehama wa  Mamlaka ya  Serikali Mtandao, Khadija Mzenzi wakati alipotembelea banda la maonesho la mamlaka hiyo alipomwakilisha  Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kilele cha Wiki ya Utumishi wa Umma  kwenye Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma, Juni 23, 2025. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama nyaraka za Maendeleo ya Watumishi  kwa Mwaka zilizoandikwa kwa lugha ya kiswahili  alipotembelea mabanda ya maonesho  wakati alipomwakilisha  Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kilele cha Wiki ya Utumishi wa Umma  kwenye Viwanja vya Chanangali jijini Dodoma, Juni 23, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza alipomwakilisha  Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kilele cha Wiki ya Utumishi wa Umma  kwenye Viwanja vya Chanangali jijini Dodoma, Juni 23, 2025.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)