Happy Lazaro, Arusha 
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa  ,John Mongela ametoa rai kwa  jumuiya ya Umoja wa wazazi  kupata muda wa kutosha wa kuwaelewesha wananchi kutambua  umuhimu wa amani, mshikamano na utulivu  uliopo ndani ya Taifa.
 Ametoa rai hiyo Kwa niaba ya Katibu Mkuu wa CCM Balozi Emmanuel Nchimbi wakati akifungua kongamano la kumpongeza  Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Suluhu Kwa kutimimiza  miaka minne ya  mafanikio katika uongozi wa Taifa.
 “Mafanikio ni kitu kimoja lakini Amani na mshikamano  huu umechangia Kwa kiwango  kikubwa sana  kupata maendeleo haya” amesema.
Amesema kuwa katibu Mkuu balonzi nchimbi ameeilekeza Jumuiya ya Wazazi kulibeba swala la  kukamasisha  amani na mshikamano  pamoja na kuwa mfano   wa kudumisha amani ,ulinzi na usalama   katika maeneo  yao hasa katika kipindi hiki  tunapoelekea  katika uchaguzi.
“Tudumishe Amani ulinzi na usalama katika maeneo yetu  hata kama tutategeshewa Ili tuweze kugafilika na kuingia kwenye fujo sisi tuwe imara na kuepuka vishawishi hivyo haswa katika kuelekea uchaguzi tuwe mfano wa kuimarisha amani ” amesema.
Aidha amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassani ameasisi  falsafa ya R4 ambayo ni lazima watanzania wote tuidumishe Kwa ajili ya kuimarisha zaidi maendeleo  na utulivu wa Taifa letu.
 Kwa upande wake  Mwenyekiti wa  jumuiya ya wazazi Taifa  Fadhili  Maganya amesema kuwa   jumuiya ya wazazi inampongeza Rais Dokta Samia Suluhu Hassan Kwa kuleta maendeleo ndani ya miaka  minne tangu aliposhika hatamu za uongozi wake ikiwemo kuboresha miundo mbinu ya  Barabara,  miundombinu ya maji, miundombinu ya  Afya, ujenzi wa zahanati , na vituo vya Afya pamoja na huduma zingine za kijamii.
 Amewaomba  wananchi kumuunga mkono , kumtia moyo , kumuombea  na kumtakia kila la kheri  Dokta Samia Suluhu Hassan Kwa kuwa  yupo tayari kushughulikia  changamoto  za maisha zinazowakabili watanzania na kuzipatia ufumbuzi.
 “Mwaka huu tunauchaguzi tuhakikishe kwamba kupitia miundo yetu ya Chama Cha Mapinduzi tuhakikishe tunamuombea  tunamtetea na kumsemea Kwa wananchi” amesema  mwenyekiti
Naye  Katibu Mkuu jumuiya ya Wazazi Ally Hapi ameeleza azimio la Baraza kuu la wazazi wa Chama Cha Mapinduzi Kwa kumpongeza rais Kwa kutiza miaka minne ndani ya uongozi na kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi   pamoja na kuhakikisha falsafa ya R4 inatekelzwa wa vitendo ikiwemo umoja, mshikamano ikiwemo utekelezaji wa ilani ya CCM pamoja na maboresho kwa wananchi.
“Wajumbe wa Baraza la wazazi tumefanya kikao Cha Baraza kuu la kawaida Jijini Arusha,tumezingatia kazi nzuri alizofanya Rais ikiwemo ujenzi wa miradi ya kimkakati  ikiwemo bwawa la Mwalimu Nyerere ambapo mashine tisa you zimewsahwa ikiwemo utuaji wa ndoo kichwani “amesema .
Amesema pia  wajumbe  wa Baraza kuu walimpongeza Rais Samia Kwa kazi kubwa ya kutekeleza ilani hiyo ndani ya kipindi cha miaka minne ikiwemo kupongeza mkutano mkuu wa CCM Kwa kumchgua Rais Samia kuwa mgombes mteule wa CCM ikiwemo Jumuiya hiyo kuwa mstari wa mbele kuhakikisha ushindi huo unapatikana na jumuiya hiyo ipo tayari kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.