KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC),imeiagiza Serikali kuichunguza Kampuni ya Ujenzi inayojenga Jengo la Maabara na Makao Makuu ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) lililopo jijini Dodoma baada ya kuchelewesha mradi huo ambao ulitakiwa kukamiliki mwezi Machi 2024 lakini mpaka sasa ujezni upo asilimia 72.
Agizo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.Naghenjwa Kaboyoka,wakati wa kamati hiyo ilipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi huo.
Amesema kuwa haiwezekani Serikali imemlipa Mkndarasi lakini anaongezewa mudfa wa kumaliza mradi mara nne lazima mkandarasi hana uwezo.
“Wakandarasi kama hao hawatakiwe kupewa miradi mingine ya Serikali na kamati hiyo ya bunge kwa ujumla wataendelea kufuatilia na endapo watabaini mkndarasi huyo kapewa mradi mwingine wataihoji Serikali.
Hata hivyo Kmati hiyo imeridhishwa na Viwango vya Ujenzi wa Majengo hayo na kuwataka wasimamizi waongeze kasi ili kuhakikisha mradi unakamilika mwezi Agosti mwaka huu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Viwango nchini TBS Dkt.Ashura Katunzi,amesema mradi huo unagharimu zaidi ya shilingi bilioni 25 ulinza Machi 2022 na ulitarajiwa kumalizika Mwezi Machi 2024 na wamemuongezea muda Mkandarasi na kuagiza mradi ukamilike mwezi Agosti Mwaka huo.
Amesema uwepo wa maabara hizi utasaaidia kusogeza huduma karibu kwa wananchi kwani bidhaa zinazozalishwa kanda hii zitapimiwa hapahapa badala ya kwenda Dar es Salaam.
Dkt.Katunzi amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo kwa mkandarasi ya kuchelewesha ujenzi huku akiwa haidai chochote serikali kwani kila madai aliyokuwa akileta hulipwa kwa wakati