Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi,Innocent Bashungwa akifafanua jambo katika mkutano huo jijini Arusha leo.

Aliyeko katikati ni Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi,Innocent Bashungwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha kuhusu mkutano huo


………..
Happy Lazaro, Arusha .
NAIBU Waziri Mkuu,Dotto Biteko amesema kuwa nchi ya Tanzania ina rasilimali nyingi katika sekta ya madini na Gesi asilia na kampuni nyingi zimewekeza katika sekta hiyo, hivyo ni wajibu wa kampuni hizo kueleza kwa uwazi mapato yanayopatikana katika shughuli zao za kila siku.
Hayo yamesemwa jijini Arusha na Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi,Innocent Bashungwa wakati akizungumza kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dokta Dotto Biteko .
Ameyasema hayo katika ufunguzi wa mkutano wa 62 wa bodi wa bodi ya EITI uliofanyika katika hoteli ya Grandmelia iliyopo mkoani Arusha na kuhudhuriwa na nchi wanachama 52 Duniani.
Amesema kuwa, wananchi wa Tanzania wanataka kujua rasilimali zao za nchi zinawanufaishaje hivyo ni wajibu wa
Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika rasilimali za Madini na Gesi Asili{EITI} kuhakikisha kuwa kampuni zote zilizowekeza katika sekta hizo hapa nchini kuweka wazi mapato yake ikiwa ni njia mojawapo ya uwajibikaji.
Bashungwa amesema Tanzania imejiunga na EITI mwaka 2009 na ilikuja kubadili sheria mwaka 2015 ya kutaka kila kampuni inayowekeza katika sekta hizo kuweka wazi mapato wanayopata ili wananchi waweze kujua kwa kiasi gani rasilimali za nchi zinawanufaisha.
Bashungwa amewataka wawekezaji kuwekeza katika sekta za madini na Gesi Asilia kwa kuwa sera zake ni za uwazi na zenye manufaa na pia aliwataka wawekezaji kujikita katika sekta ya Utalii kwani sekta hiyo kwa sasa inajulikana kote nchini kufuatia filamu ya The Royal Tour ilizinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan na kutangazwa kote Duniani na kuvutia watalii wengi hapa nchini.
Amesema Rais Samia Suluhu Hassan amejenga mazingira mazuri na rafiki kwa kuwekeza hapa nchini katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya madini,Nishati na Gesi Asilia hivyo EITI inapaswa kusisitiza wawekezaji kufanya kazi kwa uwazi na uwajibikaji katika ukusanyaji mapato.
Naye Waziri wa Madini,Antony Mavunde amesema kuwa hatua ya Rais kuimarisha Diplomasia katika kipindi chake cha muda mfupi kumefanya mikutano mingi ya Kimataifa kufanyika nchini hatua ambayo serikali inanufaika na mikutano hiyo.
Mavunde amesema eneo la uwazi na uwajibikaji ni eneo nyeti kwa rasilimali za nchi hivyo ni wajibu wa wawekezaji kuweka wazi mapato yao ili wananchi waweze kujua wananufaika vipi na rasilimali zao za nchi.
Naye Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu {CAG}mstaafu,Ludovick Utouh ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bodi ya EITI amesema kufanyika kwa Kikao hicho nchini ni faida kubwa kwa nchi kwani haijawahi kutokea toka Tanzania ilipojiunga na Bodi hiyo mwaka 2009.
Amesema Bodi ya EITI hadi imetoa ripoti 14 mbalimbali hadi sasa katika utendaji kazi wao na june mwaka huu inatarajia kutoa ripoti ya 15 hivyo wanajivunia kwa utendaji wao wa kila siku na wanasisitiza uwazi na uwajibikaji kwa wawekezaji katika kila nchi.