WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii watoto na makundi maalumu ,Dkt Doroth Gwajima akizungumza katika kikao hicho mkoani Arusha .
Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Paul Makonda akizungumza katika kikao hicho mkoani Arusha leo.
……
Happy Lazaro, Arusha .
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii watoto na makundi maalumu ,Dkt Dorothy Gwajima, amesema bado kunahitajika msukumo mkubwa wa kutoa Elimu kwa Jamii katika  mikoa ya Arusha na Manyara,ambayo bado kiwango cha unyanyasaji ni kikubwa ili kujenga Jamii yenye usawa yakiwemo  makundi maalumu.
Ameyasema hayo  leo kwenye Ukumbi wa mikutano wa mkuu wa Mkoa alipokuwa akipokea taarifa ya Kamati mbalimbali za maandalizi ya maadhimisho ya siku ya wanawake Ulimwenguni Marchi 8 mwaka huu,na kusema kuwa ameridhika na maandalizi .
Amesema lengo la maadhimisho hayo ni kuonyesha nguvu ya wanawake katika uchumi hivyo kuwafuata machozi wanawake  kutokana na mifumo kandamizi zilizopo,maadhimisho hayo yakomboe fikira na hivyo kwenda pamoja ukombozi wa Jamii pasipo itikadi yeyote .
Gwajima amesema kuwa kuna watu wanatakiwa kufunguliwa kutoka  kwenye changamoto ya minyororo na hatimae kuwepo na jamii iliyoyo huru.
Amesema kuwa, Mkutano wa Dunia  uliofanyika Beijing Nchini China mwaka 1995  uliona kulikuwepo na kundi kubwa la masikini  katika nchi zinazoendelea ambapo katika miji na Vijijini umasikini upo katika sura mbili tofauti  ambapo vijijini kiwango cha umasikini ni mbaya zaidi na waathirika zaidi ni wanawake.
Gwajima ameongeza kuwa, wanawake ndio waathirika wakubwa wananyanyapaliwa wameathiriwa na shughuli  za kiuchumi,hawajui biashara na shughuli zingine wamebakia tegemezi mwenza wake akifatiki basi ndio mwisho wa maisha yake.
Amefafanua kuwa, mkutano huo wa wanawake Dunia  uliofanyika Beijing ilikuwa na maazimio 12 ,ikiwemo kuwawezesha wanawake kiuchumi, kuzijua haki za kisheria ,kuwawezesha kupata mafunzo ya ajira na Elimu ,kuwepo uwakilishi wa wanawake. kwenye Uongozi  kupitia majukwaa ya uwezeshaji kiuchumi.
“Kuwawezesha wanawake kisheria na Uongozi ,Elimu kwa umma na huduma kupitia jukwaa la maendeleo ya Jamii na hapa nchini kumeshaanzishwa Baraza uwezeshaji wanawake kiuchumi.”amesema
Amesema sasa ni wakati wa Wizara mbalimbali,taasisi,NGOS kuamka na kuungana pamoja kupaza sauti ili kukomesha ukatili katika Jamii.
Amefafanua  kuwa hiyo itakuwa ni kuwafuta machozi wanawake kutokana na mifumo yote kandamizi na hilo ndilo lengo la Wizara kukomesha ukatili wa kijinsia hivyo maadhimisho hayo yatumike kukomboa fikira na kwenda pamoja katika ukombozi pasipo itikadi yeyote.