Mkurugenzi Mkuu wa Shirika  la Nyumba la Taifa (NHC) ,Bw. Hamad Abdallah,akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC),Mhe. Augustine Vuma,akiongozana na wajumbe wa kamati hiyo kukagua miradi nane ya majengo ya Wizara yanayojengwa na NHC  kwa gharama ya Sh.Bilioni 186.8 katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo Oktoba 26,2024.
KAMATI  ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) wakiwa katikaziara ya  kukagua miradi nane ya majengo ya Wizara yanayojengwa na NHC  kwa gharama ya Sh.Bilioni 186.8 katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo Oktoba 26,2024.
KAMATI  ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) wakiwa katikaziara ya  kukagua miradi nane ya majengo ya Wizara yanayojengwa na NHC  kwa gharama ya Sh.Bilioni 186.8 katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo Oktoba 26,2024.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika  la Nyumba la Taifa (NHC) ,Bw. Hamad Abdallah,akitoa maelezo kwa
 Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) ilipofanya ziara ya kukagua miradi nane ya majengo ya Wizara yanayojengwa na NHC  kwa gharama ya Sh.Bilioni 186.8 katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo Oktoba 26,2024.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) ,Mhe. Augustine Vuma,akizungumza na waandishi wa habari  leo Oktoba 26,2024  mara baada ya  kukagua miradi nane ya majengo ya Wizara yanayojengwa na NHC Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC,Bw. Hamad Abdallah,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) kutembelea na  kukagua miradi nane ya majengo ya Wizara yanayojengwa na NHC Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
          
       Muonekano wa Jengo la Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi linalojengwa na Shirika  la Nyumba la Taifa (NHC) katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Na. Alex Sonna-DODOMA
KAMATI  ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) imeridhishwa na kasi ya ujenzi wa majengo kwenye Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma  ambayo Shirika  la Nyumba la Taifa (NHC) ni mkandarasi na kusisitiza ikamilike kwa wakati uliopangwa.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Mhe. Augustine Vuma,ameyasema hayo leo Oktoba 26,2024 wakati wa ziara ya kamati hiyo ya kukagua miradi nane ya majengo ya Wizara yanayojengwa na NHC  kwa gharama ya Sh.Bilioni 186.8 katika Mji huo na yanatarajiwa kukamilika Januari 31, 2025
Amesema kamati hiyo imeridhishwa na mwenendo wa utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa majengo katika mji wa Kiserikali Mtumba unaotekelezwa na shirika la Nyumba la taifa (NHC).

“Tumeona majengo mengi hatua za ujenzi zipo zaidi ya asilimia 80 na wapo ndani ya mkataba waliowekewa na tunaamini watakamilisha ndani ya muda uliopangwa, na miradi hii itaipa nguvu NHC ijiendeshe kwa tija zaidi, naipongeza Bodi kwa usimamizi mzuri wa shirika hili ambalo tunaona limefanya mageuzi makubwa yenye tija,”amesema Mhe.Vuma

Kuhusu utunzaji wa majengo, Mwenyekiti huyo amesema kuwa serikali imewekeza fedha nyingi kwenye ujenzi wa majengo kwenye Mji huo na yapo mbioni kukamilika hivyo ni vyema kuangalia namna ya kutunza vizuri.

“Huu Mji kwasasa unang’aa na serikali imetumia mabilioni kuujenga, baada ya muda Fulani utakutana na uchakavu majengo yatakuwa hayang’ai kama yanavyong’ara kwasasa, majengo mengi ya serikali yamekuwa yakijengwa na kukamilika vizuri baada ya muda ukienda unakuta miundombinu yote ya maji, majitaka na muonekano wa jengo inakuwa ni changamoto,”amesema.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa NHC,Bw. Hamad Abdallah, amesema ili sekta ya Nyumba nchini iweze kupata ustawi mkubwa serikali inapaswa kuendelea kushawishi sera inayoleta unafuu wa kodi kwenye vifaa vya ujenzi na kuondoa kodi ya ongezeko la thamani kwenye nyumba za gharama nafuu.

“Wanunuzi wa nyumba za NHC ambao ni mmoja mmoja hawawezi kurejesha VAT kwa sababu hawafanyi biashara, mwaka jana serikali ilifanya maamuzi mazuri sana kwa nyumba zote ambazo thamani yake haizidi Sh.Milioni 50 zinaondolewa VAT na hilo linafanyika.”

“Lakini sisi tuna kiu ya kuona kuwa walau wanunuzi wote wa nyumba waondolewe hiyo kodi kwa kuwa shirika litakuwa limelipa kodi zote za serikali zinazohitajika ili kuwafanya watanzania wamudu kulipa fedha zinazohitajika kwenye ununuzi wa nyumba,”amesema Bw.Abdallah

Aidha, amesema kuwa kwasasa serikali imefanya vizuri kwenye sekta ya kilimo ambapo mikopo yao ni kwa riba ndogo na kupendekeza kamati iishauri serikali kuangalia namna ya kuwawezesha watanzania wanaochukua mikopo ya nyumba wapate kwa riba ndogo.

“Haya yote tumewasilisha kwa kamati wameyabeba kwa kuwa mengine ni ya kisera ili kuangalia ni kwa kiwango gani riba zitapungua ili watanzania waondokane na upangaji waingie kwenye umiliki wa nyumba,”amesema