
Happy Lazaro,Arusha .
Arusha .Watoto wenye mahitaji maalumu hususani wasiosikia (viziwi) wanakabiliwa na changamoto ya kutokuelewa darasani na kuishia kufeli kutokana na walimu wengi wanapofundisha kutokutumia lugha ya alama.
Aidha changamoto hiyo imekuwa ikipelekea kiwango cha kufeli kwa watoto hao kuendelea kuwa juu kutokana na kutokuelewa chochote wanapokuwa darasani na hata kwa wazazi wake pia.
Hayo yamesemwa mkoani Arusha na Mkurugenzi wa Taasisi inayotafsiri maandishi mbalimbali kwa lugha ya alama (BILAT) (TSLTDO ) Sensor Msimbete wakati akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 30 ya elimu jumuishi iliyofanyika mkoani Arusha .
Msimbete amesema kuwa changamoto hiyo huchangiwa na baadhi ya walimu wanaowafundisha pamoja na wazazi wanaoishi nao kutokufahamu lugha za alama kwani mtoto anatakiwa pindi anapozaliwa anakutana na lugha hizo akiwa mdogo ili aweze kuzoea mazingira.
“Changamoto hizo zote wanazopitia wenzetu tunazijua kwani na sisi tumepitia humo ndio maana tumeamua kuja na taasisi hii inayotafsiri maandishi mbalimbali kwa lugha ya alama BILAT (TSLTDO) kupitia programu ya BLOOM ambayo tumeanzisha sisi ili kuwezesha watoto hao waliopo ngazi ya chekechea hadi chuo kikuu waweze kupata elimu wanayostaili kwa kutumia vitabu mbalimbali vilivyotafsiriwa kwa kutumia lugha ya alama na kuweza kujitegemea baadaye na imeonyesha mafanikio makubwa sana kwa viziwi “amesema Msembete.
Aidha amefafanua zaidi kuwa,ni jukumu la.serikali kuwapatia bajeti kwa ajili ya kuendelea na zoezi hilo la kutafsiri vitabu mbalimbali kwa lugha ya alama ili viweze kusambazwa mashuleni na vyuoni na hivyo kuwawezesha wanafunzi hao kuweza kuelewa zaidi na kuongeza kiwango cha ufaulu mashuleni.
“Hadi sasa hivi tumeshatafsiri vitabu sita ambavyo vitaweza kutumika katika elimu.ya chekechea ambapo tumekuwa tukitumia programu ya BLOOM katika kufanya kazi hiyo na lengo ni kutafsiri kuanzia elimu.ya awali hadi vyuo vikuu ila tunaomba serikali itupatie bajeti kwa ajili ya kuendelea na shughuli hiyo ili na wenzetu waweze kuelewa madarasa kupitia vitabu hivyo “amesema .
Msimbete.