Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo Agosti 1, 2024 amemwakilisha Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Miaka 70 wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) inayofanyika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma.
Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Pindi Chana, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi, pamoja na Wanachama wa Chama cha Wanasheria Tanganyika.
Kaulimbiu: “Miaka 70 ya kuwepo kwa Tanganyika Law Society”.