Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) imepongezwa kuendelea kuvisimamia Vyama vya Ushirika na kufanikiwa katika kuhamasisha Ushirika kwenye Sekta mbalimbali na Makundi Maalumu.

Wakizungumza na Jambo Tv baadhi ya wananchi waliotembelea banda la Tume ya maendeleo ya Ushirika kwenye maonesho ya 48 Biashara ya Kimataifa kupata elimu kuhusiana na kazi zinazofanywa na TCDC walisema mabadiliko chanya yanayoonekana kwa sasa ni kutokana uongozi madhubuti uliopo pamoja na nguvu kubwa iliyowekwa katika usimamizi.

” Unapata iman kubwa na kinachoelekezwa katika mabanda kuhusu Ushirika nahii nikutokana na misingi mikubwa iliyowekwa”Alisema juma kitundu.

Aidha vyama vya Ushirika vimeimarika na Wananchi wengi wanaendelea kujiunga navyo katika Sekta za Kilimo, fedha, Madini, Nyumba na Mifugo