NJOMBE,Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Gwakisa Kasongwa pamoja na Mwenyekiti wa chama cha Msingi cha Ushirika cha Isowelo Amcos kilichopo kata ya Mtwango wilayani Humo wameiomba wizara ya Kilimo kupitia programu ya jenga kesho Bora BBT kuwasaidia wakulima wa viazi kulifikia soko lenye tija la Somalia ambalo roba moja ya Viazi inauzwa zaidi ya 200,000 badala ya kuendelea elfu 65000/= jijini Dar es salam na mtwara.

Kissa ametoa ombi hilo kwa mratibu wa mradi wa BBT na afisa masoko wa mradi huo kutoka wizara ya Kilimo wakati wakikagua shughuli ya mavuno na kisha kupeana elimu ya kilimo hicho katika mashamba ya Isowelo amcos ambapo vijna zaidi ya 600 wamechangamkia fursa za uchumi zilizofunguliwa na serikali ya wilaya kwa lengo la kuwakwamua vijana na wanawake kwenye wimbi la ajira na umasikini

Katika Ziara hiyo Kissa ameomba kituo cha utafiti tari kuwapa eneo la utafiti la Igeli ili kufanya shughuli za kilimo biashara cha viazi pamoja na mitaji huku menyekiti wa amcos hiyo Elia Mhonjwa akiomba masoko ya moja kwa moja katika nchi zenye uhitaji mkubwa kama somalia .

Baada ya kukagua mashamba ya ushirika na kujiridhisha na mavuno ndipo wataalamu kutoka wizara ya kilimo wanaosimamia mradi wa BBT akiwemo Vumilia Zinkankuba mratibu wa mradi wakaeneleza jinsi wanavyokwenda kusaidia vijana hao 600 kuwekeza katika kilimo cha miti,viazi na parachichi na kisha suala la masoko kwa kuingia mikataba ya biashara na wanunuzi.

Nao baadhi ya wanufaika wa mradi wa BBT uliyoanzishwa na mkuu wa wilaya ya Njombe na kisha kuungwa mkono na wizara ya kilimo,akiwemo Erick Ngole wamesema mtazamo wa mkuu wa wilaya umekuwa na maono chanya ndiyo sababu ya vijana wengi kujitokeza hususani kwenye kilimo cha viazi.