KAMISHNA  Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya nchini (DCEA) Aretas Lyimo,akizungumza  wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa waelimishaji umma kuhusu madhara ya rushwa na dawa za kulevya yaliyofanyika jijini Dodoma.
NAIBU  Mkurungezi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Neema Mwakalyelye,akizungumza  wakati wa ufungaji wa mafunzo ya siku tatu kwa waelimishaji umma kuhusu madhara ya rushwa na dawa za kulevya yaliyofanyika jijini Dodoma.
BAADHI ya washiriki wa mafunzo ya siku tatu kwa waelimishaji umma kuhusu madhara ya rushwa na dawa za kulevya yaliyofanyika jijini Dodoma.
Na. Gideon Gregory-Dodoma.
KAMISHNA  Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya nchini (DCEA) Aretas Lyimo,amesema nguzo kuu ya kukabiliana na matumizi ya dawa za kulevya na Rushwa nchini ni kutoa elimu kwa jamiii ili iwe na uelewa juu ya madhara hayo.
 Kamishna Jenerali Lyimo,ameyasema hayo  wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa waelimishaji umma kuhusu madhara ya rushwa na dawa za kulevya yaliyofanyika jijini Dodoma.
Amesema kuwa kuna  haja kwa waelimishaji umma mliopatiwa mafunzo kuwekeza nguvu kwenye utoaji wa elimu kwa wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo.

Aidha  Kamishna Jenerali Lyimo,amesema kundi hilo la wanafunzi wa shule za msingi,sekondari na vyuo kama litapatiwa elimu na kutambua madhara ya rushwa na dawa za kulevya tutakuwa na taifa lenye utulivu na uchumi imara.

“Rushwa na dawa za kulevya madhara yake yanafanana hivyo basi kama waelimishaji umma mtajikita kwenye utaojai wa elimu kwa umma mtasaidia taifa kuwa na watu wasiojihusha na rushwa au dawa za kulevya”amesema Kamishna Jenerali Lyimo

Kamishna Jenerali Lyimo,amesema kuwa  kupitia muunganiko wetu na klabu ambazo tayari tumeshanzianzisha huko mashuleni itasaidia kuwafikia kwa uharaka zaidi watu katika ngazi za mitaa hadi huko kwenye Halmashauri kwani wanafunzi wengi wanatokea huko.

Hata hivyo amesema kuwa matumizi ya dawa za kulevya yanaathari kijamii na kiuchumi kwani yanachanagia kuathiri nguvu kazi ya taifa na kuondoa utulivu wa nchi.

“Kama taifa litakuwa halina utulivu hata wawekezaji watashindwa kuja kuwekeza kutokana na matukio ya kiharifu yatokanayo na matumizi ya dawa za kulevya”amesema

Kwa upande wake Naibu Mkurungezi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Bi. Neema Mwakalyelye, amesema katika mafunzo hayo ya siku tatu washiriki wamejifunza mambo mbalimbali ikiwemo tatizo la dawa za kulevya nchini.

“Pia wamejengewa uwezo wa namna ya kupambana na dawa za kulevya na vita ya rushwa kwani biashara ya dawa za kulevya kwa sehemu kubwa inahusisha na rushwa”amesema Mwakalyelye