Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Mohammed Khamis Abdulla akizungumza wakati wa hafla ya kuwakabidhi vyeti vya ufadhili wa masomo ya muda mrefu nje ya nchi kupitia Mradi wa Tanzania ya Kidijitali awamu ya kwanza iliyofanyika leo Septemba 9,2023 jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi akizungumza katika hafla ya kuwakabidhi vyeti vya ufadhili wa masomo ya muda mrefu nje ya nchi kupitia Mradi wa Tanzania ya Kidijitali awamu ya kwanza iliyofanyika leo Septemba 9,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya, Bi. Salome Kessy akitoa taarifa ya mradi wakati wa hafla ya kuwakabidhi vyeti vya ufadhili wa masomo ya muda mrefu nje ya nchi kupitia Mradi wa Tanzania ya Kidijitali awamu ya kwanza iliyofanyika leo Septemba 9,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Ulaya na Amerika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. Gerald Mbwafu,akitoa mada wakati wa hafla ya kuwakabidhi vyeti vya ufadhili wa masomo ya muda mrefu nje ya nchi kupitia Mradi wa Tanzania ya Kidijitali awamu ya kwanza iliyofanyika leo Septemba 9,2023 jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Mohammed Khamis Abdulla (hayupo pichani) akizungumza wakati wa hafla ya kuwakabidhi vyeti vya ufadhili wa masomo ya muda mrefu nje ya nchi kupitia Mradi wa Tanzania ya Kidijitali awamu ya kwanza iliyofanyika leo Septemba 9,2023 jijini Dodoma.
KATIBU Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknoljia ya Habari Bw.Mohammed Khamis Abdullah,akiwakabidhi vyeti vya ufadhili wa masomo ya muda mrefu nje ya nchi kupitia Mradi wa Tanzania ya Kidijitali awamu ya kwanza iliyofanyika leo Septemba 9,2023 jijini Dodoma.
KATIBU Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknoljia ya Habari Bw.Mohammed Khamis Abdullah,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutoa vyeti vya ufadhili wa masomo ya muda mrefu nje ya nchi kupitia mradi wa Tanzania ya Kidijitali hafla iliyofanyika leo Septemba 9,2023 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
SERIKALI kupitia mradi wa Tanzania ya Kidijitali awamu ya kwanza 2023/24 umetoa ufadhili masomo ya muda mrefu na muda mfupi nje ya nchi kwa watumishi 500.
Hayo yamesemwa leo Septemba 9,2023 jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknoljia ya Habari Bw.Mohammed Khamis Abdullah,wakati wa hafla ya kuwakabidhi vyeti vya ufadhili wa masomo ya muda mrefu nje ya nchi watumishi wa umma wapatao 20 kutoka katika Wizara, taasisi za umma na halmashauri za miji na wilaya.
Bw.Abdullah, amesema kuwa katika ufadhili huo watumishi 50 ndiyo watakaokwenda nje ya nchi kwa ajili ya masomo ya muda mrefu na wengine 450 ni masomo ya muda mfupi.
“Niwapongeze sana nyie ambao mmekuwa katika awamu hii ya kwanza ambao idadi yenu mpo 20 kati ya watu 211 waliomba nafasi za kushiriki mafunzo haya.
“Niwasihi huko mtakapo kwenda kitu cha kwanza ni kutanguliza uzalendo wa taifa lenu na mtakacho jifunza kule lazima mkilete nchini ili kuongeza tija katika maswala ya Teknolijia ya Habari na Mawasiliano”amesema Bw.Abdullah,
Aidha amesema kuwa kupitia mradi wa Tanzania ya kidijitali serikali imepanga kujenga vyuo viwili vya TEHAMA katika mkoa wa Dodoma na Kigoma pamoja na vituo nane vya ubunifu.
“Lakini pia tunapanga kuwa na sera mpya ya TEHAMA na Ubunifu ili kuzikuza na kuzisimamia bunifu zote hivyo mkajifunze na munaweza kuwa hata wakufunzi katika vyuo vyetu vya TEHAMA ambavyo tumepanga kuvijenga”amesema
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi amesema kuwa watumishi hao wanakwenda kuongeza ujuzi na maarifa na watakaporejea ofisi hiyo itahakikisha wanatumika vizuri kitaifa na kimataifa.
Naye Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Ulaya na Amerika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Bw. Gerald Mbwafu ,amewataka watumishi hao walipata nafasi ya masomo nje ya nchi kuzingati sheria za nchi na vyuo wanavyokwenda kusoma.
Awali Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya, Bi. Salome Kessy ametoa taarifa ya ufadhili huo amesema Mradi wa Tanzania ya kidijitali umepanga kutoa ufadhili wa mafunzo kwa watumishi 500 kati ya hao watumishi 50 watapatiwa mafunzo ya muda mrefu na watumishi 450 watapatiwa mafunzo ya muda mfupi katika maeneo ya teknolojia zinazoibukia.