Katibu wa CCM Wilaya ya Mlele Joshua Mbwana akikabidhi zawadi kwa timu ya Black Scopioni FC kutoka Kijiji cha Inyonga Kata ya Inyonga aliyeibuka Bingwa wa mashindano hayo
Mlezi wa Mashindano ya haya ya Diwani wa Kata ya Inyonga Soud Mlolwa Mbogo na Katibu wa CCM Wilaya ya Mlele Joshua Mbwana wakifuatilia mtanange wa fainali ya mashindano ya Diwani cup kati ya timu ya Black Scopion na Chonile FC zote kutoka Kijiji cha Inyonga Kata ya Inyonga,
Mashabiki wakifuatilia mashindano hayo
Na Kibada ERNEST
Michuano ya Kombe la Diwani wa Kata ya Inyonga imehitimishwa kwa kumpata bingwa wa michuano hiyo kwa mwaka 2023 ambayo ni timu ya Black Scopion kwa mara nyingine tena kwa kuichapa timu ya Chonile Fc na kuibka Bingwa kwa mwaka 2023 na kujinyakulia kitita cha shilingi laki tatu na nusu huku mshindi wa pili akiwa Chonile FC ailiyojinyakulia shilingi laki tatu.
Michuano hiyo iliyokuwa inashirikisha jumla ya timu kumi na sita yamefadhiliwa na diwani wa Kata ya Inyonga Mhe.Soud Mlolwa Mbogo ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mlele.
Michuano ya Kata maarufu kwa jina la Diwani CUP imemalizika kwenye uwanja wa shule ya Msingi Inyonga huku timu ya Balack Scopioni ikiibua mshindi baada ya kuibamiza timu ya Chonile FC jumla ya magori 3-1 na kujihakikishia ubingwa kwa mara ya pili mfululizo.
Jumla ya timu 16 zilishiriki na yaliendeshwa kwa mtindo wa ligi ambapo timu zilicheza toka awamu ya kwanza kwa makundi hadi kufikia fainali, katika michuano hiyo timu iliyoibuka Bingwa ilijinyakuliwa kitita cha shilingi laki tatu na nusu taslimu fedha za kitanzania. Huku mshindi wa pili akijinyakulia shilingi laki tatu kamili na mshindi wa tatu aliondoka na shilingi laki mbili na nusu huku mchezaji bora na waamuzi bora kila mmoja akiondoka na shilingi elfu hamsini.
Diwani wa Kata ya Inyonga Mhe.Soud Mbogo ambaye ndiye Mlezi wa Michuano hiyo ameeleza kuwa lengo la kuanzisha mashindano hayo ni kuibua vipaji na kuvikuza katika Kata ya Inyonga na Halmashauri kwa ujumla ikiwa ni kutekeleza Ilani ya CCM,
Pia Mhe Mbogo ameeleza kuwa kwa sasa michezo ni ajira,michezo imewasaidia vijana wengi kupata ajira na kujiongezea kipato, vipo vipaji vingi lakini havionekana hivyo kupitia michuano hii vipaji vingi vitaibuliwa na kuonekana na vijana watanufaika kupitia vipaji vyao vya michezo. na Michuano hiyo itakuwa inafanyika kila mwaka. .
Aidha amewapongeza timu zote zilizoshiriki na hizi mbili zilizoingia fainali na kuwaomba kudumisha nidhamu na bidii waliyoionesha katika michuano hiyo, timu 16 zilishiriki lakini ni timu mbili tu zilizofanikiwa kuingia fainail hivyo labda ni kutokana na bidii waliyoinesha pamoja na nidhamu katika michezo ndiyo maana wamefanikiwa kufika hapo walipofika kwenye fainali ya michuano hiyo.
Mhe.Mbogo ameeleza kuwa michezo ni sehemu ya burudani, michezo ni sehemu ya mazoezi kuimarisha miili yao na kujenga afya ya miili yao hivyo amewaomba waendelee kushirikiana namna hiyo na wataendelea kuiboresha kila mwaka ili iweze kuwa bora Zaidi.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi mgeni rasmi katika michuano hiyo Katibu wa CCM Wilaya ya Mlele Joshua Mbwana amewaasa vijana kucheza mipira kwa nidhamu ya hali ya juu na kuwasisitiza wasicheze kwa kuumiza na kukomoona kwa kuwa uhai ni muhimu kuliko mpira wenyewe.lazima wajali kwanza uhai wao.
Mbwana amesema iwapo wataumia hata Serikali itakuwa imekosa nguvu kazi, maana ukiumia inakuwa haina maana tena kwani jamBo la msingi ni kucheza bila kukamiana kama ukiumia iwe bahati mbaya isiwe kwa makusudi.
Aidha Mbwana amewaonya waamuzi kuchezesha kwa haki ili mshindi apatikane kwa haki kweli. na wala siyo upendeleo wao.kwa kuwa waamuzi wamekabidhiwa dhamana hiyo basi watende haki Mshindi apatikane kwa haki,.kwa kuwa mashindano hayo yanatoa nafasi kwa vijana kuonesha vipaji vyao na hatimaye kujijengea mazingira mazuri ya kuonekana na timu nyingine kubwa na hata timu ya taifa.ameeleza kuwa Michuano hiyo itakuwa ikifanyika kila mwaka .