Afisa lishe mradi wa viungo shirika la PDF mkombozi Christopher akimkabidhi vifaa vya kuhifadhia vyakula mkulima wa viungo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wakulima hao juu ya mbinu Bora za utunzaji wa chakula ,hafla iliyofanyika Ofisi za viungo  Mwanakwerekwe Zanzibar 

Afisa lishe mradi wa viungo shirika la PDF mkombozi Christopher akizungumza na wakulima wa viungo kuhusiana na vifaa vya kutunzia chakula wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa wakulima hao  juu ya mbinu Bora za utunzaji wa chakula yalioambatana na makabidhiano ya vifaa hivyo,hafla iliyofanyika Ofisi za viungo  Mwanakwerekwe Zanzibar Julai 05,2023.PICHA NA FAUZIA MUSSA -MAELEZO ZANZIBAR

Na Rahma Khamis Maelezo                
Afisa Lishe katika Mradi wa Viungo Mkombozi Christopher amewataka Wanawake na Vijana kujiingiza katika kilimo hasa cha Vanila  ili kujikwamua kiuchumi.
Ameyasema  hayo huko Ofisi za Viungo  Mwanakwereke Wilaya ya Magharib B wakati alipokua akitoa mafunzo maalum kwa wakulima walio chini ya mradi wa viungo kuhusiana na mbinu bora za kuhifadhia chakula.
Amesema kuwa iwapo watajishuhulisha na kilimo hicho  kutawasaidia kupata mahitaji yao na kuwataka wakulima hao kulima hasa zao la Vanilla kwani ndio zao linalostahamili ukame.
Aidha amefahamisha kuwa mafunzo hayo ni ya awamu ya tatu kwa walimu wa Vikundi vya wakulima hao ambayo yanaelekeza jinsi ya kusarifu na kuhifadhi chakula ili kiweze kukaa kwa muda mrefu na salama  kwa matumizi ya binadamu.
Ameeleza kuwa licha ya mafunzo hayo pia wakulima hao  wamepatiwa vihifadhio vya mazao  ikiwemo  chupa za kigae 396 kwaajili ya kuhifadhia juisi ya nyanya, maboksi 1332 ya kuhifadhia mbogamboga (ZIPPERBAG)  na Vipolo  maalum vya kuhifadhia viungo (PADUU) 500.
Afisa ameongeza kwa kusema kuwa vifaa hivvyo watakabidhiwa wakulima 149 Unguja na wakulima  50 kwaupande wa  Pemba ili  kuhifadhia bidhaa zao na kuweza   kuakaa kwa muda mrefu bila kuharibika.
Nao Wakulima wa Viungo  kutoka Kizimbani na Donge Mbiji wamesema wamenufaika na mradi huo  kutokana na elimu wanazopatiwa mara kwa mara kwani wameweza kujiamini na kuweza kulima mazao na kuyachakata wenyewe.
Aidha wamefahamisha kuwa licha ya elimu walioipata , mradi  umewawezesha kulima kisasa kwa kuwapatia  miundombinu mbakimbali ikiwemo maji na kusema kuwa vifaa walivyopatiwa katika kuhifadhia vitawasaisdia kuhifadhia bidhaa zao kwa matumizi ya baadae.
Hata hivyo wamewashauri wakulima wenzao kulima kilimo cha biashara  kitakachowasaidia kutoka kimaisha.
Nae Mkulima wa Bustani za nyumbani( Kitchen Garden) kutoka Migombani Sharif Said Nambaga amewashauri wanawake na Vijana wasijiache kwa kutegemea ajira  kutoka Serikalini na badala yake  kujikita katika kilimo cha mbogamboga ikiwemo mchicha naTembere ili kujiongezea kipato.
Mafunzo hayo  ya siku moja yametolewa na mradi wa viungo chini ya ufadhili wa umoja wa ulaya kupitia mradi wa Agri-Connect na kuwashirikisha wakulima wa viungo,matunda na mbogamboga  kutoka Mjini na Vijijini.