Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Afya ya mimea na viuatilifu Tanzania (TPHPA) Profesa Joseph Ndunguru  akizungumza  jijini Arusha kuhusiana na maadhimisho  hayo. 
Julieth Laizer ,Arusha.

Arusha .Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya afya ya mimea na viuatilifu (TPHPA) ,Dokta Ndunguru  amewataka wananchi kutunza mazao yao kwa kufuata kanuni na mbinu za kudhibiti afya ya mimea ili kuweza kuongeza tija na kuchochea ajira na  kupunguza  umaskini .

Ameyasema hayo jijini Arusha wakati akizungumza katika maadhimisho  ya Afya ya mimea duniani yaliyoadhimishwa katika makao makuu ya TPHPA yaliyopo Ngaramtoni  mkoani Arusha.
Dokta Ndunguru amesema kuwa,kuna  umuhimu mkubwa wa wananchi kujiwekea dhana  ya kutunza mazao yao kwa kufuata kanuni ili yaweze  kuongeza  kipato kwao na kupata mazao ya kutosha .
Dokta Ndunguru  amesema kuwa, asilimia  80 ya chakula cha binadamu kinatoka kwenye mimea ambapo mimea yenyewe imekuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya visumbufu ,mabadiliko  ya tabi ya nchi,na uchomaji wa misitu.
Amesema kuwa,kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Afya ya mimea kwa ajili ya kupunguza  umaskini njaa na kulinda mazingira pamoja na kukuza uchumi wa nchi zetu “.
Aidha amesema kuwa,lengo kubwa la mamlaka hiyo ni kuwa na mfumo mmoja wa kudhibiti afya ya mimea na hatimaye kuweza kuondokana na changamoto  mbalimbali. 
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa afya ya mimea katika mamlaka hiyo, Dokta Benignus Ngowi amesema kuwa,wamekuwa wakihakikisha bidhaa zinazozalishwa  hapa nchini  na kwenda nje ya nchi hazina visumbufu vya mimea .
Ngowi amesema kuwa,wamekuwa wakifanya ukaguzi wa mimea   ,mazao, na vipando vyote kwa  lengo la kulinda mimea isivamiwe na wadudu  wasumbufu  ambapo wana vituo 36 mipakani  .
“Huwa tumekuwa tukifanya ukaguzi maalumu katika maeneo ya mipakani  kwani huwezi kutambua visumbufu  kwa macho ni lazima ufanye ukaguzi wa kutosha ili kujiridhisha na kuweza kuondokana na changamoto  mbalimbali.”amesema Ngowi. 
Kwa upande wake  Profesa Eliningaya  Kweka amesema kuwa, wana maabara zenye idhibati ambazo zinamwezesha mkulima kuunganishwa  na masoko ya nje na kupambana na umaskini katika kuongeza  pato la nchi. 
Amesema kuwa , wanatumia teknolojia  bora na za kisasa pamoja na mabomba ya kunyunyuzia viautilifu sambamba na kutumia ndege nyuki  kunyunyuzia  dawa.
“Tunapenda katoa rai kwa wakulima endapo wakikutana na viuatilifu ambavyo havina nembo  kutoka mamlaka hiyo wasitumie kwani zitawaletea  shida  kwenye afya zao hivyo nawaomba sana wawe makini katika hilo. “amesema Profesa Kweka.