Waziri wa Kilimo Mh. Hussein Bashe akizungumza katika uzinduzi wa Jukwaa la Mfumo wa Chakula Afrika, uliofaywa na Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu jijini Dar es Salaam leo Ijumaa 17,2023.
(PICHA NA JOHN BUKUKU-IKULU-DAR ES SALAAM)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Ikulu akifuatilia na kuandika mambo kadhaa wakati Waziriwa Kilimo Hussein Bashe (Hayupo pichani) akitoa hotuba yake leo kwenye uzinduzi huo uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo Ijumaa 17,2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdori Mpango akizunguma jambo na Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn ambaye ni Mwenyekiti AGRA wengine ni Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete katikati na kutoka kulia ni Mfanyabiashara Rostam Aziz, Rais wa AGRA Dkt Agnes Kalibata na Spika wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson.
Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania wakifuatilia mkutano huo.
Kutoka kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn ambaye pia ni Mwenyekiti AGRA akifuatiwa na Rais wa AGRA Dkt Agnes Kalibata pamoja naye ni Mfanyabiashara Rostam Aziz wakifuatilia mkutano huo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Kassim Majaliwa akisalimiana na Mfanyabiashara Rostam Aziz wakati alipowasili katika mkutano huo.
………………………………….
Na Selemani Msuya
WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe amewakaribisha wawekezaji kutoka katika maeneo mbalimbali duniani kuja kuwekeza kwenye kilimo na kuahidi kuwa Serikali itatoa ardhi na kuweka mazigira bora.
Bashe ametoa kauli hiyo ya ukaribisho leo Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na washiriki wa uzinduzi wa Jukwaa la Mfumo wa Chakula Afrika (AGRF), uliofaywa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Waziri Bashe amesema uzinduzi wa jukwaa hilo hapa nchini unaenda kufungua fursa kwenye sekta ya kilimo, hivyo ameomba wawekezaji kujitokeza ili tafsiri sahihi ya kufanyika kwa mkutano huo hapa nchini ikamilike.
Amesema Tanzania ina zaidi ya hekta milioni 29 zinazofaa kilimo cha umwagiliaji, hivyo mtu au taasisi inayotaka kuwekeza katika eneo hilo milango ipo wazi.
“Tunataka kilimo kiwe biashara, hivyo tunawaomba watu au taasisi ambazo zipo tayari kuja kuwekeza nchini, kwani kwa sasa tuna zaidi ya hekta milioni 29 zizonafaa kwa kilimo cha umwagiliaji,” amesema.
Bashe amesema lengo la Rais Samia na serikali yake ni kuona Tanzania inalisha dunia chakula safi na salama, hivyo lengo hilo linaweza kutumia kwa kuvutia wawekezaji.
Amesema mkutano wa Jukwaa la Mfumo wa Chakula Afrika unaotarajiwa kufanyika Septemba 5 hadi 9 mwaka huu nchini Tanzania utakuwa chachu kubwa ya kuhamasha kilimo.