Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ndugu Edward Mpogolo amezindua Msimu wa GS1 Tanzania wa Barcodes Day 2023 Ambayo Itafanyika kuanzia Tarehe 15 hadi 19 Juni 2023.
Msimu huu utakwenda na “Operesheni Ibua viwanda” vilevile kuhamasisha kampeni ya “Buy Tanzania Buy 620”. Msimu huo umelenga katika, kuhamasisha matumizi ya Kidigital kwa SMEs za Tanzania.
Kazi kubwa ya GS1 ni utoaji wa huduma za Barcodes, hata hivyo mwaka huu taasisi ya GS1 Tanzania imejipanga katika kuhakikisha, viwanda vyote vilivyopewa Barcodes vinachukua nafasi kubwa katika kuongeza uzalishaji na kuongeza ajira kwa wananchi nchini.
GS1 Beyond Barcodes 2023 imejikita katika kuhakikisha taasisi ya GS1 Tanzana inaunganisha nguvu na wadau wengine katika, kujenga mfumo wa viwanda vyenye matokeo makubwa kwa ajili ya kujenga Sekta Binafsi Imara.
GS1 Tanzania mwaka huu pia imepania kusimamia upelekaji wa Bidhaa za Viwanda vyenye Barcodes nje ya nchi ili kupata masoko ya kimkakati, GS1 Tanzania Barcodes Day inakwenda kuleta mabadiliko katika kuzitambulisha bidhaa za wazalishaji, wenye Barcodes kwa ajili ya matokeo makubwa.