*****************

NJOMBE

Serikali imeanza rasmi utekelezaji wa mpango utakaofikisha asilimia 100 ya kiwango cha upatikanaji wa huduma ya maji mijini nan vijijini ifikapo 2025 mkoani Njombe kwa kusaini mikataba mitano yenye thamani ya bil 2.9 na makampuni tofauti ya kitanzania ambayo inakwenda kutekelezwa katika kipindi cha mwaka mmoja katika wilaya zote nne za mkoa huo.

Mbali na mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji ,umesainiwa pia mkataba wa ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya mifumo ya majitaka katika mji wa Njombe ambao unatakajwa kukua kwa kasi kwasababu ya ongezeko wanaohamia na Kuanzisha makazi katika halmashauri hiyo.

Changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji safi imekuwa kilio kikubwa katika msimu wa kiangazi hususani maeneo ya mijini jambo ambalo limekuwa likisababisha akina mama kufata maji kwenye mito mabondeni na wengine kuchimba visima ili kuikabili hali hiyo.

Kwa kuona ukubwa wa changamoto hiyo serikali ya mkoa kwa kushirikiana na wizara ya maji zimelazimika kutoa fedha za ujenzi wa miradi mitano itakayogharimu kiasi cha bil 2.9  ambapo pindi ikikamilika inaelezwa kuja kumaliza kabisa adha hiyo.

Awali Mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka akizungumza amesema kwakuwa serikali imekusudia kutatua kero ya maji kwa kutoa mabilioni ya fedha za miradi hatopenda kuona mkandarasi akishindwa kutekeleza mradi katika muda uliyopangwa kimkataba.
“Ni matarajio yetu kuona mwaka 2025 wakazi wa Njombe kawakabiliwi na shida ya huduma ya maji kwasababu serikali imekusudia kumtua ndoo mwanamke kichwani,anasema Mtaka mkuu wa mkoa wa Njombe “
Akieleza hali ya upatikanaji wa maji kwasasa katika mkoa wa Njombe mhandisi Sadici Chaka ambaye ni meneja wa RUWASA mkoani humo anasema kwasasa mkoa unahuduma ya maji kwa asilimia 80 ambapo wakazi takribani 458,763 kutoka vijiji 273 wananufaika na huduma .
“Kwa kuwa hatujafika asilimia 100 ndiyo maana tunaongeza jitihadaza kuanzisha miradi mipya na kuboresha ya zamani ili kufikia asilimia miamoja,anasema mhandisi Sadick Chaka meneja wa Ruwasa Njombe” 

Punde baada ya kusaini mikataba hiyo ndipo mkandarasi kutoka kampuni ya NDIKA Engineering Costantine Mayombe akasema wamefika na kutazama eneo la mradi hivyo kwakuwa wamejidhatiti kiutendaji wanakwenda kutekeleza kwa ubora mkubwa  ndani ya muda uliyopandwa .
“Sisi tunauzoefu mkubwa na miradi ya maji na tuna viteakazi vya kutosha na hatuna shaka na ujenzi wa mradi huu ,tunachokiomba ni ushirikiano kwa pande zote muhimu,anasema Mayombe mhandisi kutoka kampuni ya NDIKA Engineering”
Kwa upande wake Odasan Haule kutoka kampuni ya NIPO AFRICA iliyosaini kandarasi ya ujenzi wa mradi wa mfumo wa maji taka halmashauri ya mji wa Njombe anasema kampuni yao inazaidi ya miaka 15 katika sekta ya maji hivyo wanauhakika wa kutekeleza mradi wa majitaka ndani ya muda wa mkataba uliyosainiwa.
Mbali na utekelezaji wa majukumu yao Haule ameomba serikali kutoa fedha kwa wakati na wananchi watoe ushirikiano pindi wanapohitajika ili kutimiza takwa la serikali la kutoa huduma bora kwa wananchi.
“Tunaomba mwajili ajitahidi kutoa fedha kwa wakati katika kipindi cha utekelezaji wa mradi ili wakamilishe mradi bila chhangamoto yeyote kukwamisha,anasema Odasan Haule kutoka kampuni ya NIPO Africa”
Katika hafra ya masainiano ya mikataba wamehudhuria pia wabunge na wawakilishi wa wananchi wa ngazi mbalimbali ambapo Mbunge wa Ludewa Joseph Zakarius Kamonga akamuomba mkandarasi anaejenga mradi jimboni kwake kuhakikisha anamaliza mradi badala ya kukimbia kabla haujakamilika kwani jimboni kwake kuna changamoto kubwa ya maji.
Kamonga anasema licha ya serikali kutoa fedha nyingi jimboni kwake lakini anaomba nguvu ya ujenzi wa miradi ya maji kata za mwambao mwa ziwa Nyasa kwasababu wananchi wanaliwa na mamba pindi wanaoenda kuteka maji katika mito mikubwa ukiwemo wa Luhuhu.
“Wananchi wangu wanapoteza maisha kwasababu ya maji wengi wanaliwa na mamba hivyo niwaombe wakandarasi wafanye kazi yao ili kuokoa maisha ya watu hawa,anasema Joseph Kamonga mbunge wa Ludewa”