Home Mchanganyiko NI MAKOSA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA UKOPESHAJI BILA LESENI

NI MAKOSA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA UKOPESHAJI BILA LESENI

0

********************

Benki Kuu ya Tanzania imebaini kuwa kuna baadhi ya taasisi, kampuni
na watu binafsi wanaojihusisha na biashara ya kutoa mikopo bila ya kuwa
na leseni, jambo ambalo ni kinyume na Kifungu cha 16(1) cha Sheria ya
Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018.

Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuutaarifu Umma kuwa taasisi,
kampuni na mtu binafsi wasio na leseni husika hawaruhusiwi kufanya
biashara ya kukopesha.

Aidha, kwa mujibu wa Kifungu cha 16(2)(a) cha
Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018, hatua
zitakazochukuliwa kwa ukiukaji wa Sheria hiyo ni pamoja na faini
isiyopungua Shilingi Milioni 20 au kifungo kwa muda usiopungua miaka
miwili.

Sambamba na tangazo hili, Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuwaasa
wananchi kuepuka kukopa au kufanya biashara na taasisi, kampuni au
mtu binafsi ambao hawana leseni.

Aidha, orodha ya taasisi, kampuni na
watu binafsi wenye leseni za biashara ya kukopesha zilizotolewa na Benki
Kuu ya Tanzania inapatikana kwenye tovuti ya Benki Kuu ambayo ni
www.bot.go.tz.