Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akitoa nasaha zake mbele ya waumini wanawake katika Maulid ya kumsifu Mtume Muhamad S.A.W yaliyosomwa katika Madrasatul Mushawar Mwembeshauri Jijini Zanzibar.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi (wa pili kushoto) akikaribishwa na wakinamama wa Madrasatul Mushawar Mwembeshauri katika Maulid ya kumsifu Mtume Muhamad S.A.W yaliyosomwa leo katika masjid Mushawar Mwembeshaur Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi (wa pili kushoto) akiitikia dua ya Ufunguzi wa Maulid ya kumsifu Mtume Muhamad S.A.W iliyosomwa na Bi.Asha & Bi.Uchungu (wa Pili kulia) katika Masjid Mushawall Mwembeshauri Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi leo,ambayo yameandaliwa na Madrasatul Mushawar Mwembeshauri .
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi (wa pili kushoto) akifukizwa udii wakati wa kumswalia Mtume Muhammad S.A. katika Maulid yaliyosomwa leo katika Masjid Mushawall Mwembeshauri Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi,ambayo yameandaliwa na Madrasatul Mushawar Mwembeshauri .
Wamamadrasatul Mushawar Mwembeshauri wakimswalia Mtume Muhammad S.A.W katika Maulid yaliyosomwa Masjid Mushawall Mwembeshauri Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi leo Mgeni Rasmi alikuwa Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi (hayupo pichani).ambapo madrasa mbali mbali zimealikwa katika hafla hiyo.
Waumini Wanawake kutoka sehemu mbali mbali wakiitikia Maulid ya kumsifu Mtume Muhamad S.A.W yaliyosomwa leo katika Masjid Mushawall Mwembeshauri Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi,ambayo yameandaliwa na Madrasatul Mushawar Mwembeshauri .[Picha na Ikulu