Mkimbiaji wa Riadha kwa upande,wa wanawake katika mita 100 kwa wenye umri kuanzia miaka 50 kutoka Timu ya Ras Arusha Melania Kapungu akichanja mbuga kumaliza mbio hizo na kujinyakulia medali ya Dhahabu ya michezo ya Shimiwi mkoani Tanga picha na Prisca Libaga Maelezo Tanga.
***********************
Na Prisca Libaga Maelezo Tanga
Timu ya Ras Arusha imeshika nafasi ya kwanza katika mchezo wa riadha mita 100 baada ya mkimbiaji wake Melania Kapungu kushinda katika michezo ya Shimiwi inayoendelea.
Melania akiongea Mara baada ya kuibuka na ushindi huo kwa upande wa wanawake wenye umri kuanzia miaka 50 na kupata medali ya dhahabu amesema kwamba alijipanga kushinda kwa kupokea maelekezo kutoka kwa wakufunzi wake.
Michezo ya Shimiwi mwaka huu inayofanyika Mkoani Tanga imekuwa na mvutano wa kila timu kutaka kuibuka na ushindi na kuwa kivutio kwa wakazi na mashabiki wa michezo mkoani Humo.Hata hivyo kwenye Riadha mkoa wa Arusha umeendelea kufanya vizuri huku wakimbiaji wake wakiendelea kujipanga kuendelea kujikusanyia medali katika michezo hiyo.
Nae Kapungu ameendelea kutoa wito kwa wafanyakazi kujitokeza kupenda michezo bila kujali umri wao kwani kufanya hivyo ni sehemu ya kupambana na magonjwa yasioambukiza ambayo yameshika kasi nchini hivi sasa.
Amesema michezo ni sehemu ya kuondoa msongo wa mawazo kujenga afya na utimamu wa mwili hivyo kila moja katika maeneo yao wawe mabalozi wazuri wa kuitangaza michezo kwani ni ajira kwa watoto wetu.