***********************

NA EMMANUEL MBATILO

 KLABU ya Simba imefanikiwa  kuinyuka timu  ya Primeiro de Agosto Fc  kwa mabao 3-1 mchezo ambao ulipigwa kwenye nchini Angola hivyo nakuwa na faida kwa Simba ambaye atasubiri kucheza mchezo wa marudiano ili aweze kufuzu hatua ya makundi.

Simba Sc iimepata mabao kupitia kwa wachezaji wake Clautos Chama, Israel Mwenda pamoja na mshambuliaji wao hatari Moses Phiri.

Simba Sc ilianza kupata bao la  kwanza dakika za mwanzo kipindi cha kwanza kupitia kwa  kiungo  wao Chama na kuwapeleka mapumziko wakiwa mbele kwa bao  1-0.

Bao la timu  ya Primeiro de Agosto Fc lilifungwa dakika za lala salama kupitia kwa mkwaju wa penati.