Mratibu wa Umoja wa Mataifa (UN) Zanzibar Dorothy Temu Usiri akifanyiwa vipimo vya sindikizo la damu (BP) wakati wa matembezi maalum ya kuhamasisha afya ya akili ikiwa ni shamrashamra kuelekea maadhimisho ya siku ya akili Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Oktoba 10,hafla iliyofanyika Kinazini Mjini Zanzibar.
Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Andemichael Ghirmy akifanyiwa vipimo vya sindikizo la damu (BP) wakati wa matembezi maalum ya kuhamasisha afya ya akili, ikiwa ni shamrashamra kuelekea maadhimisho ya siku ya akili Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Oktoba 10,hafla iliyofanyika Kinazini Mjini Zanzibar.
Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Afya Duniani Zanzibar (WHO) Andemichael Ghirmy akiwapatia muongozo wa matembezi maalum ya kuhamasisha Afya ya akili wadau mbalimbali wa Afya kabla ya kuanza kwa matembezi hayo ya umbali wa kilomita tano yalioambatana na mazoezi ya Viungo na Upimaji wa Afya ikiwa ni shamrashamra kuelekea maadhimisho ya siku ya Afya ya Akili Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo oktoba 10, hafla iliyofanyika Kinazini Mjini Zanzibar.
Wajumbe wa Umoja wa Mataifa (UN), watendaji wa Wizara ya Afya na wadau mbali mbali wa Afya wakitembea umbali wa kilomita tano kuhamasisha Afya ya akili ,ikiwa ni shamrashamra kuelekea maadhimisho ya siku ya Afya ya akili Duniani ambayo huadhimishwa Oktoba kumi ya kila mwaka,matembezi hayo ya kilomita tano yalianzia Kinazini kuelekea Malindi ,Vuga ,Michenzani kupitia Mlandege na kumalizikia Kinazini .
Wajumbe wa Umoja wa Mataifa (UN), watendaji wa Wizara ya Afya na wadau mbali mbali wa Afya wakifanya mazoezi ya viungo mara baada ya kukamilika matembezi ya kilomita tano kuhamasisha Afya ya akili ,ikiwa ni shamrashamra kuelekea maadhimisho ya siku ya Afya ya Akili Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Oktoba 10,hafla iliyofanyika Kinazini Mjini Zanzibar.
Meneja Kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma Zanzibar Hamad Bakar Magarawa akizungumza na wadau wa Afya mara baada ya matembezi yaliyoambatana na mazoezi ya Viungo na upimaji wa Afya kuhamasisha Afya ya akili ,ikiwa ni shamrashamra kuelekea maadhimisho ya siku ya Afya ya Akili Duniani inayoadhimishwa kila ifikapo Oktoba kumi, hafla iyofanyika Kinazini Mjini Zanzibar.
Mratibu wa Umoja wa Mataifa (UN) Zanzibar Dorothy Temu Usiri akizungumza na wadau wa Afya mara baada ya matembezi maalum yaliyoambatana na mazoezi ya Viungo na upimaji wa Afya kuhamasisha ya Afya ya akili ,ikiwa ni shamrashamra kuelekea maadhimisho ya siku ya Afya ya Akili Duniani inayoadhimishwa kila ifikapo Oktoba kumi,hafla iyofanyika Kinazini Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt.Salim Slim akizungumza na wadau wa Afya mara baada ya matembezi maalum yaliyoambatana na mazoezi ya Viungo na upimaji wa Afya kuhamasisha ya Afya ya akili ,ikiwa ni shamrashamra kuelekea maadhimisho ya siku ya Afya ya Akili Duniani inayoadhimishwa kila ifikapo Oktoba kumi, hafla iyofanyika Kinazini Mjini Zanzibar.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akili Zanzibar Dkt. Khadija Abdul-rahman akizungumza wadau wa Afya mara baada ya matembezi maalum yaliyoambatana na mazoezi ya Viungo na upimaji wa Afya kuhamasisha ya Afya ya akili ,ikiwa ni shamrashamra kuelekea maadhimisho ya siku ya Afya ya Akili Duniani inayoadhimishwa kila ifikapo Oktoba kum, .hafla iyofanyika Kinazini Mjini Zanzibar. PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR
……………………………
Na Rahma Khamis Maelezo –Zanzibar
Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Salim Slim amesema ni vyema jamii kuweka mfumo madhubuti wa kufanya mazoezi ili kujikinga na maradhi mbalimbali ikiwemo magonjwa ya Afya ya Akili.
Ushauri huo ameutoa huko Kinazini mara baada ya kumaliza matembezi maalum ya kuunga mkono siku ya Afya ya Akili Duniani yanayofanyika kila mwaka ifikapo oktoba 10 ikiwa ni shamrashamra kuelekea siku hiyo.
Amesema kuwa ili mtu awe na Afya nzuri lazima awe na mfumo mzuri wa kufanya mazoezi kwani bila ya kufanya hivyo,mfumo wa damu utakua mzito na kupelekea kupata madhara ya kupoteza kumbukumbu.
“Ikiwa hatufanyi mazoezi katika maisha yetu angalau kwa dakika 20 kwa kila siku damu itaganda na kuweza kushindwa kufanya kazi vizuri baada ya hapo kinachofuata ni maradhi kutokana na kuganda kwa damu katika miili yetu”,alisema Dkt Slim.
Aidha amefahamisha kuwa mfumo wa kufanya kazi kwa kujiacha unaathiri mwenendo wa afya katika jamii,hivyo kila mtu aangalie hali ya maisha kwa kufanya mazoezi kwa mujibu wa hali ya Afya aliyonayo.
“Wafanya kazi wengi siku hizi wamejiacha sana kwani kila mtu anatumia usafiri sehemu ndogo usafiri uwe wa binafsi au daladala hii ni sababu kubwa inayopelekea watu kupata maradhi,”alisema Dokt huyo.
Hata hivyo Dokt Slim amewashukuru wadau wa afya kutoka ( UN) kwa kuleta wazo la kuanzisha mazoezi kwani kufanya hivyo kunaboresha afya ya binadamu.
Nae Daktari dhamana wa Kitengo cha Magonjwa ya Akili Hospitali ya Kidongochekundu Khadija Abdulrahman amesema kuwa mazoezi yana uhusiano mkubwa na afya ya Akili katika maisha ya kila siku.
Amefahamisha kuwa watu wengi katika jamii hasa wafanyakazi hukaa muda mrefu bila kufanya mazoezi, kati yao wanakua na msongo wa mawazo hivyo kufanya mazoezi kutawasaidia kuondosha vichochezi vya magonjwa ya Akili na mengine ikiwemo kisukari na shindikizo la damu.
Aidha ameisa jamii kutobweteka na kujitahidi kubadilika kwa kufanya mazoezi ili kupunguza ongezeko la maradhi ya Afya nchini.
Nao wadau wa Afya kutoka Umoja wa Mataifa (UN) wamesema kuwa wameamua kufanya hivyo ili kuhamasisha jamii kushiriki katika kufanya mazoezi ili kuimarisha Afya ya Akili na kujikinga na maradhi mbalimbali.
Aidha wamefahamisha kuwa kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani mtu mmoja kati ya wanne Ulimwenguni kote anaishi na tatizo la Afya ya Akili , hivyo ni wajibu wakila mmoja kufanya mazoezi ili kujiepusha na tatizo hilo.
Matembezi ya kilo mita tano yaliyoambatana na mazoezi ya viungo na upimaji wa Afya yameandaliwa na wadau wa Afya Zanzibar ikiwemo WHO, UNICEF na UNDP ambapo matembezi hayo yameanzia Kinazini kuelekea Malindi Vuga,Mnzimmoja Michenzani na kurejea Kinazini.