RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiondoa pazia kuashiria kuufungua Msikiti wa Masjid Mubarak Kiboje Muembeshauri Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo 7-10-2022, baada ya ufunguzi huo amejumuika na Wananchi katika Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid hiyo. (Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuashiria kuufungua Msikiti wa Masjid Mubarak Kiboje Muembeshauri Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo 7-10-2022,na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe.Rashid Hadidi Rashid na (kushoto kwa Rais) Msimamizi wa ujunzi wa Msikiti huo Shikh.Mohammed Hamdan Mohammed, baada ya ufunguzi huo amejumuika na Wananchi katika Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid hiyo. (Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akishiriki kuitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi(kulia kwa Rais) na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Rashid Hadidi Rashid na (kushoto kwa Rais) Katibu Mtendaji Ofisi ya Mufti Zanzibar Sheikh.Khalid Ali Mfaume.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimia na Viongozi wa Kamati ya Masjid Mubarak Kiboje Muembeshauri Wilaya ya Kati Unguja, alipowasili katika viwanja vya Masjid hiyo kwa ajili ya ufunguzi wa Msikiti huo na kujumuika katika Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika leo baada ya ufunguzi wake na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe Rashid Hadidi Rashid.(Picha na Ikulu)
USTADH.Ali Hassan Abdalla akisoma risala ya Kamati ya Masjid Mubarak Kiboje Muembeshauri Wilaya ya Kati Unguja wakati wa ufunguzi wa Msikiti huo uliofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi na kujumuika na Wananchi wa Kijiji hicho katika Sala ya Ijumaa iliyofanyika leo 7-10-2022.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwasalimia Wananchi wa Kijiji cha Kiboje Muembeshauri Wilaya ya Kati Unguja baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa na ufunguzi wa Msikiti huo wa Masjid Mubarak Kiboje Muembeshauri leo 7-10-2022.(Picha na Ikulu)