Mkuu wa Mkoa wa Geita Bw. Martin Shigella akifanya mahojiano na Bi. Domina Rwemanyila Afisa habari Shirika la Nyumba la Taifa NHC mjini Geita.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Bw. Martin Shigella akiurahia jambo na baada ya kufanya mahojiano na Bi. Domina Rwemanyila Afisa habari Shirika la Nyumba la Taifa NHC mjini Geita.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Bw. Martin Shigella akiwa katika picha ya pamoja na baada ya kufanya mahojiano na Bi. Domina Rwemanyila Afisa habari Shirika la Nyumba la Taifa NHC mjini Geita.
.……………………………………..
Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigella ameliomba Shirika la Nyumba la Taifa – NHC kwa ajili ya kujenga jengo kubwa la biashara ili kuweza kupunguza adha ya upatikanaji wa huduma za mbalimbali kwa Wafanyabiashara na Wajasiriamali wa Mkoa huo.
Amesema kuwa kwa sasa katika mji wa Geita kuna uhitaji wa jengo kubwa la biashara ambalo litakuwa na huduma mbalimbali ambazo zitapatikana kwa wakati mmoja litasaidia kupunguza adha kwa wananchi ya kutoka eneo moja kwenda eneo jingine kwa ajili ya kupata huduma na kuongeza kuwa jengo hilo litakuwa kitega uchumi kizuri kwa NHC na Taifa kwa ujumla.
Mhe. Shigella ameyasema hayo leo asubuhi ofisini kwake wakati wa mahojianao na mwandishi wetu aliyetaka kujua lengo na madhumuni ya kuwa na Maonesho ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini kila mwaka na tija wanazopata wananchi wa Geita na Mikoa jirani kupuia Maonesho hayo.
‘Kwanza niwapongeze sana NHC kwa kazi kubwa mnayofanya ya kuendelezza makazi nchini na kujenga majengo makubwa ya biashara hii inaoensha dhahiri kuwa mnaunga mkono jitihada za Rais wetu wa Awamu ya Sita Mama Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha mnaongeza makazi kwa wananchi.
Nimuombe Ndugu yangu Nehemiah Mchechu alete timu yake ije ichangamkie fursa ya uwekezaji katika mji wetu kwani niko tayari kupitia Halmashauri kuwapatia eneo bure ili mje muwekeze maana mji wa dhahabu huu unakuwa kwa kasi kubwa sana” Alisema Shigella
Aliongeza kusema kuwa Mkoa wa Geita unakuwa kwa kasi kubwa sana kutokana na kwamba unapokea wageni wengi sana wakubwa kwa wadogo wakiwemo wafanyabiashara wa madini ambao wakati mwingine inaonekana kwao ni kero kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali, sasa kama NHC itaweka jengo kubwa hapa la biashara litasaidia kupunguza kadhia hii na hivyo kuweza kuwasaidia wananchi pia kupata huduma kwa urahisi katika eneo moja ambalo litakuwa na mabenki, maduka makubwa ya biashara na Super Market.
Katika hatua nyingine Mhe. Shigella ameiomba NHC kuendelea na mpango wake wa kujenga nyumba za makazi katika mji wa Geita kufuatia uhitaji wa nyumba hizo kuwa mkubwa kwa sasa kutokana na watumishi wengi wa kwenye migodi ni wageni hivyo uhitaji wa ngumba ni mkubwa sana.
“Mji wa Geita kuna wachimbaji wengi wa madini wakubwa kwa wadogo ambao wengi wao wanahitaji kupata nyumba za makazi, hivyo basi NHC mnaweza kuja kuzungumza na wachimbaji hawa mkaona ni kwa namna gani mnaweza mkawasaidia kwa kuwapatia makazi bora, kwani baadhi yao wanahangaika sana kupata nyumba za gharama nafuu name najua NHC inatoza gharama ndogo sana katika bidhaa zake hivyo tuwasaidie hawa ili waweze kuepukana na kadhia ya nyumba” Alisema Shigella.
Amesisitiza kuwa mradi wa SAMIA HOUSING ambao utaanza kutekelezwa katika eneo la Kawe jijini Dar es Salaam na baadaye kusambaa sehemu mbalimbali nchini, mradi huo unaweza pia kutekelezwa katika mji wa Geita kwa kujenga walau nyumba kadhaa ili Geita mnao wanufaike na mradi huo ambao unaonekana unalengo la kuwasaidia watu wenye kipato cha chini na kati.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa wa Geita amelishukuru Shirika la Nyumba la Taifa kwa kushiriki katika Maonesho ya Teknolojia ya Madini kwa mwaka wa pili mfululizo na kusema kwamba ushiriki wa NHC unatoa fursa kwa wananchi kulifahamu vyema Shirika lao na kufahamu miradi ambayo inatekelezwa kwa sasa.
Shirika la Nyumba la Taifa kwa mara ya pili mfululizo linashiriki Maonesho ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika viwanja vya EPZA Bombambili mjini Geita yanayoongozwa na Kauli mbiu isemayo “Madini na Fursa za Uchumi, Ajira kwa Maendeleo Endelevu”