Waziri wa maliasili na utalii Balozi Dk Pindi Chana akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha juu ya maandalizi ya mkutano jijini Arusha
************************
Julieth Laizer, Arusha.
Arusha.RAIS wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ,Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufungua mkutano wa 65 wa shirika la utalii duniani -Kamisheni ya Afrika (UNWTO -CAF) ambalo Tanzania ni mwanachama wake tangu mwaka 1975 utakaofanyika oktoba 5 hadi 7 jijini Arusha.
Hayo yamesemwa leo jijini Arusha na Waziri wa maliasili na utalii ,Balozi Dk Pindi Chana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha.
Balozi Chana amesema kuwa,mkutano huo unatarajiwa kukutanisha mawaziri wenye shamans ya maswala ya utalii na maliasili kutoka nchi wanachama wa UNWTO wa kanda ya Afrika zaidi ya 50 kujadili kuhusu mustakabali wa ustawi wa maendeleo ya sekta ya utalii barani Afrika hasa baada ya athari za mlipuko wa janga la UVIKO -19 iliyokuwa imeathiri utalii wa Tanzania.
Amesema kuwa,mkutano huo utahusisha wadau wengine wakiwemo watalaamu wa utalii na ukarimu katika ngazi ya kimataifa na kikanda, watoa huduma mbalimbali katika mnyororo wa utalii,wawekezaji, pamoja na watu mashuhuri zaidi ya 150.
“Kauli mbiu ya mkutano huu ni Rebuilding Africa’s Tourism Resilience for Inclusive Socio-Economic Development “na utahudhuriwa na Katibu Mkuu wa shirika hilo Zurab Pololikashvili “amesema Dk Chana.
Ameongeza kuwa,Tanzania ilichanguliwa kuwa mwenyewe wa mkutano wa 65 wa UNWTO kupitia mkutano wa 64 uliofanyika septemba 2021 nchini Cabo Verde .
Amefafanua kuwa, katika mkutano huo patafanyika matukio mbalimbali ambayo ni pamoja na jukwaa la uwekezaji kwa ajili ya kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo nchini na uzinduzi wa Investment Guideline(Tourism doing Business)Marketing Symposium kwa ajili ya kuwajengea uwezo wadau wa utalii kuhusu maswala ya masoko .
Amesema kuwa,kulingana na sera ya Taifa ya utalii (1999) mkutano huo ni muhimu kwa kuwa ni mojawapo ya jitihada za serikali katika kuongeza idadi ya watalii na kupanua wigo wa mazao ya utalii nchini kupitia uendelezaji wa mazao ya utalii ya kimkakati hususani wa mikutano na matukio .
Balozi Dk Chana amesema kuwa ,mkutano huo utawezesha kujengea uwezo watalaamu na wadau wa utalii katika kutangaza utalii,kuendeleza na kufungamanisha mazao ya utalii katika kanda mbalimbali za utalii nchini kulingana na shabana ya kuongeza idadi ya watalii kufikia watalii milioni 5 na mapato ya Dola za Marekani Bilioni 6 ifikapo mwaka 2025.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Arusha ,John Mongela amesema kuwa,mkoa umejipanga kikamilifu kuhakikisha mkutano huo unaofanyika salama na wananchi wa Arusha wananufaika kupitia mkutano huo .
Aidha Mongela amesema kuwa mkutano huo utatoka fursa sio kwa wanaarusha tu bali dunia na Afrika kwa ujumla kwani juhudi zilizofanywa na Rais za kutangaza utalii kupitia filamu ya Royal Tour ni kubwa sana na linapaswa kuungwa mkono.